Jumla ya wanafunzi 2117 sawa na asilimia 81 wameripoti katika shule za sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani.
Hayo yasemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Neema Maghembe wakati anazungumza kwenye kikao cha Wakuu wa Shule zote za Msingi na Sekondari wa Halmashauri hiyo kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile na kufanyika kwenye ukumbi wa sekondari ya Maposeni mji mdogo wa Peramiho.
Kikao hicho kililenga kupata taarifa ya kuandishwa na kuripoti wanafunzi wa Darasa la Awali, Darasa la kwanza na Kidato cha kwanza 2024 .
Mkurugenzi huyo amesema juhudi zaidi zinaendelea kufanyika ili kuhamasisha wazazi na walezi kupeleka watoto shuleni.
“Tunaendelea kuwatafuta wanafunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza nyumba kwa nyumba ili wote wafike shule”,alisisitiza Maghembe.
Mkurugenzi huyo amewataja jumla ya wanafunzi 4480 wa darasa la Awali sawa na asilimia 97 wameandikishwa na wanafunzi 4536 wa darasa la kwanza sawa na asilimia 99 wameripoti Shuleni.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amepongeza jitihada zinazofanywa na wakuu wa Shule ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji ulisababisha kuongeza idadi ya wanafunzi wa Awali, darasa la kwanza na Kidato cha kwanza.
Hata hivyo Ndile Amesisitiza kuwa wanafunzi wote wenye sifa na waliofaulu kuingia kidato cha kwanza, wafike shuleni.
Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan inatoa Elimu bure kuanzia Awali, Msingi na Sekondari
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.