MKOA wa Ruvuma umepokea mgao wa jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 10 ya fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na UVIKO -19 (mradi na 5441-TCRP).
Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Hakimu Mafuru akitoa taarifa hiyo amesema mgao huo wa fedha kwaajili ya vyumba 448 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8 kwaajili ya Shule za Sekondari,vyumba 52 katika vituo shikizi za shule ya Msingi zaidi ya shilingi bilioni moja na mabweni matatu yenye thamani ya shilingi milioni 240.
Amesema kupitia mpango huo wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 jumla ya wanafunzi 28,356 sawa na asilimia 73.1 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2021 na wameingia kidato cha kwanza mwaka 2022.
“Utekelezaji wa mradi huo wanafunzi wote waliopangiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2022 hawakukabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa ”.
Hata hivyo amesema mgao wa vyumba vya Madarasa katika Shule za Sekondari H ikiwemo Halmashauri ya Madaba vyumba 17 jumla ya shilingi milioni 340,Halmashauri ya Mbinga mgao wa vyumba vya Madarasa 88 zaidi ya Shilingi bilioni 1,Mbinga Tc mgao wa vyumba vya Madarasa 34 Shilingi milioni 680.
Halmashauri ya Namtumbo vyumba vya Madarasa 80 zaidi ya Shilingi bilioni moja Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa vyumba vya mdarasa 44 ilighalimu shilingi milioni 880 ,Halmashauri ya Songea 46 shilingi milioni 920,Songea manispaa vyumba 26 Milioni 520,Tunduru 113 zaidi ya bilioni 2.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 13,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.