Na Hope Midelo,Songea
Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo amezindua rasmi kanuni mpya za uongezaji wa virutubishi kwenye vyakula Mkoani Ruvuma,
Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Chandamali uliopo Manispaa ya Songea na kuwasilishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud S. Kigahe, kwa niaba ya Waziri Jafo.
Mhe. Kigahe amesema kanuni hizi ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha lishe bora kwa kila Mtanzania kwa maendeleo endelevu ya nchi.
Amefafanua kuwa kanuni hizo zinasimamia vyakula vinne vikuu: unga wa mahindi, unga wa ngano, mafuta ya kula na chumvi, ambavyo sasa ni lazima kuongezwa virutubishi kabla ya kuuzwa sokoni.
Serikali, amesema, imeweka mazingira rafiki kwa wazalishaji ili kuwawezesha kutekeleza kanuni hizo kwa ufanisi bila vikwazo vya kiuzalishaji.
Aidha, ametoa wito kwa wazalishaji wote nchini kuzingatia kanuni hizo kwa lengo la kuhakikisha chakula kinachozalishwa kinakuwa na ubora wa hali ya juu kwa afya ya wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.