• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ZOEZI la Sensa Tunduru linaendelea vema

Imewekwa kuanzia tarehe: August 24th, 2022


BAADHI ya wananchi waliokuwa wanasafiri kutoka wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi,wameipongeza Serikali kwa namna ilivyoratibu vizuri zoezi la sensa ya watu na makazi iliyoanza leo nchini kote.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao waliokutwa wakihesabiwa katika kituo kikuu cha mabasi mjini Tunduru walisema,sensa ya mwaka huu itafanikiwa kutokana na hamasa kubwa iliyofanywa na Serikali ambapo wananchi wengi wamepata uelewa umuhimu ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Ali Mnonjela,ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwekeza nguvu kubwa ili kufanikisha zoezi hilo muhimu  na kuwaomba wananchi ambao bado hawajahesabiwa kujiandaa na kutoa ushirikiano kwa makarani walipoewa dhamana ya kutekeleza zoezi hilo.


“mimi nimehesabiwa hapa kituo cha mabasi wakati najiandaa kwenda  Dar es slaam,utaratibu huu haujawahi kufanyika kabisa kwa miaka ya nyuma,naiomba serikali yetu iendelee kusimamia mipango mingine  ya maendeleo kama ilivyofanya kwenye zoezi hili”alisema.

Naye Hidaya Hausi,ameipongeza serikali kwa kuwajali watu wenye dharura wakiwamo wasafiri kwa kuwapatia nafasi ya kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi la mwaka 2022.


Hidaya,ameishauri Serikali  kuongeza muda ili  zoezi hilo lifanyike zaidi ya wiki moja  kwa ajili ya kutoa nafasi kwa  wananchi wenye changamoto na dharura mbalimbali wapate nafasi ya kushiriki na kupata haki yao ya msingi.


Naye mkazi wa kijiji cha Majimaji wilayani humo Swalehe Kalonga alisema, sensa ya mwaka huu imefanyika kisomi zaidi na amependa namna makarani walivyojipanga katika kuuliza maswali ya msingi yanayohusu kaya zao,hali ya kipato,ulemavu na elimu na  tofauti  na miaka ya nyuma ambapo maswali yalikuwa machache na hayakuwapa nafasi kubwa  wananchi kutoa taarifa zao muhimu.


Msimamizi wa sensa ya watu na makazi wa wilaya ya Tunduru Enock Kabakaki ambaye aliambatana na  baadhi ya makarani alisema, zoezi limekwenda kama lilivyopangwa na kuwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa makarani watakaopita katika maeneo yao.

Alisema,zoezi hilo limeanza usiku wa saa 6 na dakika 1 kwa kupita katika maeneo yote yanayohitaji kujaza dodoso maaluma kama vile vituo vya mabasi,nyumba za kulala wageni na maeneo wanayoishi watu wasio na makazi maalum.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro alisema, kwa ujumla  zoezi la sensa katika wilaya hiyo limeanza vizuri ambapo kazi kubwa imefanyika kwa makarani kupitia katika maeneo  mbalimbali ikiwamo nyumba za kulala wageni.


Alisema,makarani 1,392 ambao wamesambazwa katika vitongoji vyote 1,175 na tangu asubuhi zoezi lililopoanza  hadi sasa  hakuna changamoto yoyote  iliyojitokeza na kuwataka wananchi ambao bado hawajahesabiwa kujiandaa kushiriki na kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.


Alisema,wananchi katika vijiji mbali mbali wanatambua kwamba wana jambo lao na haliwezi kufanikiwa kama hawatajitokeza kwa wingi  kuhesabiwa  kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi linalofanyika mwaka huu.

MWISHO.



Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.