• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

Wasichana 71% Wapatiwa Chanjo Kuzuia Saratani ya Shingo ya Uzazi Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: April 30th, 2019

ASILIMIA 71 YA WASICHANA RUVUMA WAPATIWA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI 

Songea, 30 Aprili, 2019

Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kutoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 kwa asilimia 71 ya lengo kwa mwaka 2018

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alisema chanjo hiyo ilianza kutolewa mwezi Aprili mwaka 2018 katika halmashauri nane za Ruvuma.

Alitoa taarifa hiyo jana mjini Songea wakati wa kikao cha kamati ya Afya ya Msingi mkoa kutathamini zoezi la utoaji chanjo hii kwa viongozi wa mkoa na halmashauri zote

Pololet alisema lengo la chanjo hiyo ni kuwakinga mabinti dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi ambayo inaongoza kwa  vifo vya akina mama nchini.

“Wasichana umri wa miaka 14 waliochanjwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi mkoa wa Ruvuma ni 14,786 sawa na asilimia 71 ya lengo la kuchanja wasichana 16,631 sawa na asilimia 80” alisema Pololet

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Jairy Khanga alisema changamoto zilizojitokeza  wakati wa zoezi hata mkoa kushindwa kufikia lengo la asilimia 80 ni pamoja na imani potofu kwenye baadhi ya maeneo kuwa chanjo hii inaweza kuzuia mabinti kuzaa

Ametaja halmashauri za Tunduru,Namtumbo na Madaba kufanya vibaya kwenye utoaji wa chanjo hii kutokana na viashiria vya  uwepo wa imani potofu kwenye jamii hivyo wasichana kutojitokeza kupata chanjo

Dkt.Khanga alizitaja halmashauri zilizofanya vizuri mwaka huu kuwa ni Mbinga DC (100%) na Nyasa (83%)

“Serikali imeridhia chanjo hii kutolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 baada ya kufanya utafiti kujiridhisha kutokuwa na madhara kwa watu “ alisema Dkt.Khanga

Dkt.Khanga alitoa wito kwa viongozi wa dini na mila kwenye mkoa wa Ruvuma kusaidia kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hii kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha ubora wake katika kudhibiti saratani ya mlango wa kizazi.

Kwa mujibu wa Dkt Khanga , vifo 403,000 vilitokea nchini Tanzania kwa mwaka kutokana na saratani ambapo saratani ya mlango wa kizazi kwa akinamama iliachangia asimilia 37.

“Saratani ya shingo ya uzazi Tanzania  inaathiri zaidi ya (37%),saratani ya matiti (12%) na saratani ya koo (6.7%) ndio maana serikali ikaja na mkakati wa kuzuia isiendelee “ alisisitiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Katika kikao hicho cha tathmini mkoa uliazimia kuhakikisha unafanya ufuatiliaji wa mabinti waliokwisha chanjwa kujua maendeleo yao na kuhuisha taarifa za halmashauri.

Wito umetolewa pia kwa viongozi wa wilaya kuendelea kuhamasisha wananchi kuhusiana na chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kupitia vyombo vya habari na sanaa katika maeneo yao

 Mwisho

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • SERIKALI yaanza kutekeleza mradi wa kituo cha afya Mbaha

    July 01, 2025
  • RC RUVUMA azindua kituo cha mabasi Lundusi Songea

    July 01, 2025
  • MTO Ruvuma mboni ya uhai na maajabu ya utalii kuisni mwa Tanzania

    June 30, 2025
  • SERIKALI yatoa bilioni 3.4 kumaliza kero ya maji Tunduru

    June 29, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.