• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MTO Ruvuma mboni ya uhai na maajabu ya utalii kuisni mwa Tanzania

Imewekwa kuanzia tarehe: June 30th, 2025

Kuna mito duniani ambayo hukumbukwa kwa kuwa chanzo cha maji na Kuna mito mingine hujulikana kwa kuwa mpaka wa nchi

Miongoni mwa mito adimu duniani inayobeba hadhi ya kipekee kama chemchemi ya maisha, historia, utalii na urithi wa taifa ni Mto Ruvuma,ambao unapuliza pumzi ya uhai kwa mikoa ya Ruvuma na Mtwara na kuwa chombo cha amani kwa nchi jirani ya Msumbiji.

Ni mto uliobeba kila aina ya hadithi: uzuri wa asili, mandhari ya kupendeza, fukwe za kuvutia, wanyama pori, maporomoko ya kusisimua, visiwa vya asili, na hata hadithi za vita ya ukombozi wa Afrika ya Kusini.

Mto unaobeba Mkoa mzima wa Ruvuma

Kwa mujibu wa Deborah Mwakanosya, Mratibu wa Utalii Kanda ya Kusini, Mto Ruvuma ni zaidi ya mto  ni uti wa mgongo wa Mkoa wa Ruvuma kwa sababu Ndiyo mto pekee unaopita katika wilaya zote tano za mkoa wa Ruvuma ambazo ni Songea, Mbinga, Nyasa, Namtumbo na Tunduru.

Huo ndio mto mrefu kuliko yote Afrika Mashariki, ukiwa na urefu wa kilometa zaidi ya 800, ukianzia katika milima ya Matogoro Manispaa ya Songea kwenye kisima kidogo chenye mfereji mwembamba na kusafiri hadi Bahari ya Hindi.

“Kisima hicho kipo juu ya meta 1,500 kutoka usawa wa bahari, lakini kinapozalisha maji hayo ya mwanzo ya Mto Ruvuma, hayawezi kufananishwa na kazi kubwa yanayokwenda kufanya mbele,” anasema Mwakanosya kwa msisimko wa kipekee.

 

Maajabu ya asili yaliyosheheni fukwe na maporomoko

Katika wilaya ya Tunduru, Mto Ruvuma unapita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya mazingira asilia ya Mwambesi, ambapo fukwe za kuvutia na visiwa vya asili huonekana kama mchoro wa msanii mahiri.

 Katika eneo hilo, watalii huogelea, hupiga picha, huendesha mitumbwi na kushuhudia wanyama wa kila aina  kuanzia tembo na simba, hadi mamba na samaki wa ajabu.

Ndani ya hifadhi hiyo hiyo, yapo maporomoko ya ajabu ya maji yanayojulikana kama Maporomoko ya Sunda ambako huonekana ndege mdogo zaidi duniani, anayeitwa pantiole, anayekula samaki akiwa hai huku akiogelea ndani ya mto.

Nguvu ya maji inayozalisha umeme na ajira

Safari ya Mto Ruvuma haikomi kwenye mandhari bali  Katika eneo la Tulila wilayani Mbinga, maji ya mto huo yamegeuzwa kuwa chanzo cha nishati safi ya umeme kupitia mradi wa umeme wa maji unaoendeshwa na watawa wa Kanisa Katoliki. Hapo, megawati tano huzalishwa na kulisha vijiji vinavyozunguka.

Aidha, katika wilaya ya Songea, mto Ruvuma unapita katika shamba kubwa la kahawa la AVIV  lenye ukubwa wa hekta 2,000, ambapo hekta 1,000 zimetumika kwa uzalishaji wa kahawa,linatoa ajira za kudumu 1,400 na ajira za msimu 5,000.

 ambako zaidi ya wafanyakazi 3,000 wamepata ajira kupitia kilimo cha umwagiliaji  kwa kutumia njia ya matone ya Mto Ruvuma.

Utalii wa kihistoria, vita ya majimaji na uhuru wa Afrika

Si vivutio vya asili pekee vinavyohusiana na Mto Ruvuma.

Historia ya Tanzania na ukombozi wa Afrika Kusini inalindwa pia na mto huu. Maji ya Mto Ruvuma yalitumika katika Vita ya Majimaji dhidi ya ukoloni wa Kijerumani (1905–1907).

Eneo la Sunda lilibeba mapambano ya vita ya Golira War – mapigano ya msituni yaliyosaidia kuikomboa Msumbiji.

Kwa mujibu wa Mwakanosya, eneo la Negomano nchini Msumbiji, ambapo mito ya Ruvuma na Rujenda hukutana, lilikuwa ngome ya wanamapambano dhidi ya ukoloni wa Kireno.

 Mpaka wa Tanzania na Msumbiji ni Mto Ruvuma, na eneo hilo pia linaelekeza kwenye Hifadhi ya Taifa ya Niassa ya pili kwa ukubwa nchini Msumbiji.

Daraja la Umoja: Mlango wa kuunganisha mataifa

Katika Wilaya ya Nanyumbu,mkoani Mtwara mto Ruvuma umepambwa kwa daraja la kipekee lenye urefu wa meta zaidi ya 700 Daraja la Umoja, linalounganisha Tanzania na Msumbiji kupitia Kituo cha Uhamiaji cha Mtambaswala.

 Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano wa Kituo hicho Mwamba Lihami, eneo la darajani hilo lina mvuto wa kipekee kielimu na kijiografia ni makutano ya mito miwili, Ruvuma na Rujenda, na majimbo mawili ya Msumbiji ambayo ni Delgado na Niassa.

Ruvuma hadi Baharini – safari ya maji yasiyokoma

Mto Ruvuma unaendelea kupitia wilaya ya Masasi hadi eneo la Msimbati, Mtwara  mahali ambapo maji yake yanamwaga kwenye Bahari ya Hindi.

 Hapo ndipo Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma ilipoanzishwa mwaka 2000, ikiwa na eneo la zaidi ya kilometa 650 za mraba.

Mhifadhi wa hifadhi hiyo, Devis Orio, anaeleza kuwa eneo hilo lina hazina kubwa ya viumbe wa baharini na nchi kavu kuanzia samaki wa kipekee hadi viumbe wa matumbawe.

Mto wa maisha na matumaini kwa vizazi vijavyo

Mto Ruvuma pia ni chanzo cha miradi ya maji inayowanufaisha maelfu ya wakazi wa vijiji vya wilaya za Masasi na Nanyumbu.

Mradi mkubwa wa maji kutoka Mto Ruvuma umeazishwa katika vijiji vya  Masuguru na  Chipingo.

Mto Ruvuma  ni  mzizi wa maendeleo, kitovu cha utalii, mlango wa historia ya ukombozi, na kielelezo cha uzuri usio na kifani wa kusini mwa Tanzania.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MTO Ruvuma mboni ya uhai na maajabu ya utalii kuisni mwa Tanzania

    June 30, 2025
  • SERIKALI yatoa bilioni 3.4 kumaliza kero ya maji Tunduru

    June 29, 2025
  • KIWANDA kikubwa cha mbolea kitakachowanufaisha wakulima Ruvuma chazinduliwa

    June 29, 2025
  • RAS Ruvuma ateta na viongozi wa NHIF

    June 26, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.