Watumishi Wa Umma Kuweni Na Subira Ongezeko La Mishahara - Waziri Mkuu Majaliwa
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa mwanzoni nchi ilikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hewa ambapo wote kwa pamoja walikuwa wakilipwa mishahara na posho mbalimbali hivyo, ili kuwatambua watumishi halali Serikali iliamua kufanya uchunguzi na kuwagundua watumishi hao hewa.
Pia, Serikali ilifanya uchunguzi mwingine wa kuwatambua watumishi wenye vyeti stahiki vya kufanya kazi mbalimbali Serikalini kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa baada ya kumaliza utambuzi wa watumishi halali, Rais Dkt. Magufuli aliunda Tume ya Mishahara na Motisha kwa ajili ya kufanya mapitio ya kada zote za Utumishi wa Umma na viwango vya mishahara ili kutambua ulinganifu kati ya stahiki ya mshahara na kada husika.
"Lengo la Rais Magufuli kuunda tume hiyo ni kufanya tathmini nzuri ili kutambua weledi wa kazi, uwajibikaji na tija inayopatikana mahala pa kazi, hivyo baada ya kukamilika Serikali itatoa taarifa," alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa rai kwa Watumishi wa Umma kuendelea kuiamini serikali kwani ina nia ya dhati kuhakikisha watumishi wote wanapata haki zao stahiki vile vile mpaka sasa mjadala kati ya Serikali na Vyama vya Wafanyakazi unaendelea vizuri
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.