SEKTA YA MALIASILI NA UTALII.doc
6.1.5 SEKTA YA MALIASILI
6.1.5.1 Taarifa ya Misitu -
6.1.5.1.1 Utangulizi
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya eneo la km267,550 ambalo kati ya hizo km263,968 ni ardhi na km23,582 ni maji yanayojumuisha ziwa Nyasa, mito na Mabwawa. Eneo la misitu ya asili ya miombo peke yake ni km241,567 sawa na asilimia 65 ya eneo lote la ardhi.
Misitu ya Hifadhi ya vijiji iliyohifadhiwa katika wilaya zote tano (05) ni 39 yenye jumla ya eneo la km230,110.7 au Hekta 311,069.47 sawa na asilimia 7.5 ya misitu ya miombo iliyopo mkoa wa Ruvuma.
6.1.5.2 Hali ya Ufugaji Nyuki ya Mkoa
Mkoa una lengo la kuwa na mizinga 80,000 angalau kila Halmashauri iwe na mizinga 10,000 na kuwa na viwanda vya kuchakata mazao ya nyuki 20 mpaka ifikapo mwaka 2025. Utekelezaji wa lengo hili utashikisha Wakala wa Huduma za Misitu, Halmashauri, Taasisi za Umma (kama Magereza, JKT, Mashule, Vyuo) na Taasisi za Kiserikali (kama CARITAS, PALMS, Vikundi mbalimbali na wananchi kupitia miradi ya FORVAC, SECAD na wakulima wa Soya, Alizeti, Ufuta, Mawese n.k.)
Mpaka sasa mkoa wa Ruvuma una jumla ya mizinga 14,426, kati ya hiyo ya kisasa ni 10.004 na mizinga ya kienyeji ni 4,422 sawa na asilimia 30.65. Mizinga hiyo inazalisha asali kilo 16,186 wastani kila mzinga unazalisha kilo 1.12 badala ya kilo 10, uzalishaji huu hauridhishi kabisa.
Mkoa unapendekeza juhudi za kuhamasisha wananchi kushiriki zaidi kufuga nyuki kwenye maeneo ya mashamba yao hasa kwenye maeneo ya kilimo cha mazao ya Mafuta (Block farms) ya Soya, Alizeti, Ufuta na Mchikichi kwa kufanya Hivyo wananchi wataongeza mazao yao kwa sababu yatachevushwa na nyuki.
Asali itakayopatikana itawasaidia wakulima kupata kipato na chakula, Hivyo kuboresha lishe kwa Watoto wao. Ili kuleta ufanisi kwenye elimu ya ufugaji nyuki, teknolojia ya uchakataji na taarifa za masoko ni vyema kila wilaya ikaanzisha Jumuiya (Association) ya Wafugaji na wafanyabiashara wa mazao ya Nyuki. Kwa kufanya Hivyo kutatengeneza mtiririko wa taarifa za masoko na teknolojia mpya ngazi ya Kimataifa, Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya hadi Kijijini.
6.1.5.3 Hali ya Misitu na Mazao ya Misitu
Hali ya misitu ya Hifadhi ya vijiji bado sio nzuri sana kwa sababu ya uvamizi na kufanya shughuli za kibinadamu kama kulima, kuchungia, kuvuna mazao ya misitu bila utaratibu na migogoro ya mipaka kati ya wananchi na hifadhi.
Mpaka sasa wananchi bado hawajafaidika na misitu hiyo, basi ni vyema sasa juhudi zikaogezwa za kuhakikisha mazao ya misitu kama mbao zinatumika kwenye miradi ya mikakati ya Kitaifa kama Ujenzi wa madarasa, mabweni, zahanati, madawati na thamani za maofisini ili kupunguza gharama kwa wananchi.
Aidha, kwa upande wa Nyasa bado wavuvi wanatumia mitumbwi ya kuchonga magogo ambayo huoza haraka kwenye maji, huwa midogo na haina nafasi wala balance ya kutosha na kusababisha wavuvi kushindwa kuvua mbali na kuleta ajali.
Hivyo ni vyema mradi ukaelekeza nguvu Nyasa ya kutumia mbao nzuri kutengeneza maboti imara ya kudumu ili Ziwa Nyasa liweze kuleta tija.
Zao lingine linalopatikana ni mianzi ambayo kwa mkoa wetu litatumika kwa ajili ya pombe, kutengeneza makapu, matenga n.k. Sasa umefika wakati wa kutumia mianzi kibiashara ili iweze kuongeza kipato kwa wananchi kwa kupatiwa mashine ya kutengeneza njiti za meno na mishikaki, kwani njiti hizo zinatoka China na kuuzwa Mbinga na Nyasa ambako kuna mianzi mingi badala ya wananchi wetu kuzitengeneza wenyewe.
Misitu ya asili ya Ruvuma bado ina mazao mengine ya chakula kama uyoga, matunda pori, dawa za asili na baadhi ya wadudu kama kumbikumbi na senene. Mazao hayo kama yangefanyiwa utafiti na kuongezwa thamani yangeweza kutoa mchango mkubwa kwenye kuondoa umaskini na kuongeza lishe kwa wakinamama na Watoto.
Mkoa utashirikiana na wadau wengine wa ufugaji nyuki kama:
FORVAC, WWF, SUA, Chuo cha Maliasili Jamii, TFS, TAWA na TAN
6.1.5.4 Mradi wa Panda Miti Kibiashara
Mkoa wa Ruvuma uliainisha hekta 80,235 kwenye maeneo kumi na moja ya kupanda miti ya biashara kwenye wilaya za Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru. Kwenye awamu ya kwanza ya miaka kumi iliyoanzia mwaka 2015 hadi 2025, Mkoa ulikuwa na lengo la kupanda hekta 40,500 (Eka 100,000) ya biashara aina ya Misindano (Pine), Milingoti (Eucalyptus) na Misaji (Teak).
Utekelezaji wa mradi wa upandaji miti ya biashara mpaka sasa ni kama ifuatavyo:
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Hekta 7,397
Mashule na Vyuo (SUA) Hekta 1,475
Wananchi (TGA) Hekta 26,360
Halmashauri (LGAS) Hekta 1,340
Jumla Hekta 36,572
Jumla ya hekta 36,572 za miti ya biashara zimeshapandwa kwenye awamu ya kwanza sawa na asilimia 90.3 ya lengo.
Jedwali Na. 35: Idadi ya miche ya miti ya biashara na vyanzo vya maji
Wilaya
|
Bustani
|
Idadi na aina ya Miti |
||
Mashamba ya MitiTFS
|
Wananchi
|
Vyanzo vya maji
|
||
Songea
|
Wino
Mkongotema Ifinga SUA Matogoro Ndongosi Songea boys Songea girls Mahenge Nurseries |
600,000
48,000 200,000 430,000 200,000 |
200,000
10,000 300,000 30,000 32,000 |
200,000
85,000 |
Mbinga
|
Kinaha
|
|
200,000
|
95,000
|
Nyasa
|
Mpepo
Liuli |
150,000
500,000 |
10,000
50,000 |
20,000
|
Tunduru
|
Kazamoyo
|
280,000
|
100,000
|
|
Namtumbo
|
|
|
|
150,000
|
JUMLA
|
|
2,408,000
|
932,000
|
550,000
|
Jedwali Na. 36 Maeneo Maalum ya Upandaji Miti na Wananchi
Wilaya
|
Eneo
|
Matumizi
|
Aina ya miti
|
Idadi ya miti
|
Songea
|
Wino TGA
Mkongotema TGA Ifinga TGA Bonde la Luhira Lihuhu Intake Mlima Gumbiro Kibandisi Intakes Mhimbasi Intakes Lihanje Intakes Mashuleni |
Mashamba ya miti mto nguzo
Mashamba ya miti Vyanzo vya maji Vyanzo vya maji Vyanzo vya maji Vyanzo vya maji Vyanzo vya maji Mashamba ya miti |
Pine/Eucalyoptis
Pine/Eucalyptis Pine/Eucalyptis Migwina/Minyonyo |
285,000
|
Mbinga
|
Liumbe TGA
Kihangi mauka TGA Mikiga hill |
Mashamba ya miti
(Mbao, Nguzo) Mashamba ya miti (Mbao, Nguzo) Mashamba ya miti (Mbao, Nguzo) |
Pine/Eucalyptis
Pine/Eucalyptis Pine/Eucalyptis |
200,000
|
Nyasa
|
Liuli escapement
Upolo TGA |
Mashamba ya miti
Mashamba ya miti |
Teak
Pine |
150,000
|
6.1.5.5 Hifadhi ya Vyanzo vya Maji
Jedwali Na. 37: Orodha ya vyanzo vya maji vinavyotakiwa kuhifadhiwa haraka
Halmashauri
|
Kijiji
|
Chanzo kilipo
|
Kazi zinazotakiwa kufanyika
|
1. Mbinga DC
|
Kigonsera
|
Halale intake
|
Demarcation & Tree planting
|
|
Lasau
|
Lisau intake
|
|
|
Kibandai Asili na Kihongo
|
Langiro intake
|
|
|
Kiyaha
|
Kiyaha intake
|
|
|
Matiri
|
Mtende intake
|
|
Halmashauri
|
Kijiji
|
Chanzo kilipo
|
Kazi zinazotakiwa kufanyika
|
|
Kibanga
|
Kimbanga
|
Demarcation & Tree planting
|
|
Mahilo Asili
|
Liwingu
|
Demarcation & Tree planting
|
|
Miyau
|
Liwingu
|
|
|
Amanimakoro
|
Mikeke
|
|
|
Mkako
|
Halale
|
|
|
Mpapa
|
Likwela
|
|
|
Kindimbajuu
|
Mbugani
|
|
|
Ndongosi
|
Namswea
|
|
|
Wukiro
|
Wukiro
|
|
|
Ruanda
|
Namswea
|
|
|
Litoho
|
Liwanga/Ulolela
|
|
|
Kipapa na Mahilo
|
Kingoro A
|
|
|
Utili
|
Utili
|
|
|
Kagugu
|
Maganagana
|
|
|
Maganagana
|
maganagana
|
|
|
Kihungu
|
Kihungu
|
|
|
kilimani
|
Kilimani
|
|
|
Mkwaya
|
Mkwaya
|
|
|
Lupilo
|
Lupilo
|
|
|
Mateka
|
Mateka
|
|
|
Tanganazomba
|
Ugano
|
|
|
Mbangamao
|
Ukimo
|
|
|
Kikolo
|
Kikolo
|
|
|
Mpepai
|
Mpepai
|
|
2. Tunduru DC
|
Amani
|
Nambango
|
|
|
Nalasi
|
Kagoya
|
|
|
Milonde
|
Namalowe na Mwinda
|
|
|
Naluwale
|
Naluwale
|
|
3. Songea DC
|
Liula
|
Livengwa intake
|
Demarcation & Tree planting
|
|
Mbingamhalule
|
Liula intake
|
Demarcation & Tree planting
|
|
Mgazini
|
Lunyera intake
|
Demarcation & Tree planting
|
|
Kilagano
|
|
|
4. Madaba DC
|
Magingo
|
Mgombasi intake
|
Demarcation & Tree planting
|
Halmashauri
|
Kijiji
|
Chanzo kilipo
|
Kazi zinazotakiwa kufanyika
|
|
Matetereka
|
Kitekago intake
|
demarcation &Tree planting
|
|
Mahanje
|
Kibandis intake
|
demarcation &Tree planting
|
5. Namtumbo DC
|
Luhimbalilo na Naikesi
|
|
Tree planting
|
|
Njalamatata/Luegu
|
Chanzo cha Luegu
|
|
|
Rwinga
|
Chanzo cha Lwinga
|
|
6. Nyasa
|
Makata
|
Makata intake
|
Tree planting
|
|
Litindoasili na Lumecha
|
Matogoro intake
|
Tree planting
|
6.1.5.6 Utalii
6.1.5.6.1 Vituo vya Taarifa za Vivutio vya Utalii
Ili kukuza sekta ya utalii na kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali Thomas laban ameagiza kwanza, kuanzishwa kwa vituo vya taarifa za utalii kila Halmashauri.
Vituo hivyo vitakuwa chini ya Afisa maliasili na mazingira wa Halmashauri husika.
Kituo cha Namtumbo kitaanzishwa na TANAPA (Nyerere National Park) kanda ya Kusii kwa kushirikiana na Halmashauri ya Namtumbo na Tunduru kitaanzishwa na hifadhi ya mazingira asili ya Mwambesi (TFS) na vitakuwa kwenye Ofisi za Maliasili za Halmashauri za wilaya na watashirikiana na WMA zote 5 na kukianzisha (Nalika, Chingole, Mbarang’andu, Kisungule na Kibanda)
Kituo cha taarifa za vivutio vya utalii cha Mkoa wa Ruvuma
Kituo hiki kitaanzishwa na Mkoa kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Kituo hiki kitaanzishwa kwenye Ofisi za maliasili mahenge na baadae itajengwa Ofisi kubwa ambayo itakuwa na ofisi zote za sekta ya maliasili na utalii (TANAPA, TAWA, TFS, Makumbusho ya Taifa na Kituo cha taarifa cha utalii).
Kituo hiki jumuishi (onestop centre) kitahudumia hata mikoa mingine ya Tanzania.
Kituo kingine maalum kitakuwa Mbambabay ambacho TAWA watashirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Nyasa kukianzisha kwa sababu bandari ya Mbambabay ni lango kubwa la kuingia watalii toka Malawi, Msumbiji na nchi za SADC.
Taarifa zitakusanywa ni pamoja na utalii wa kihistoria, utamaduni, dini, hifadhi za wanyamapori, samaki, misitu na fukwe za maziwa, bahari na mito mikubwa kama Ruvuma na milima, kilimo na chakula cha asili.
6.1.5.7 Wanyamapori
6.1.5.7.1 Hifadhi ya Mbambabay
Hifadhi ya Wanyamapori ya Mbambabay ina jumla ya hekta 597 ikiwa ni milima miwili (Mlima Mbamba hekta 440 na Mlima Tumbi hekta 110) na visiwa viwili (Lundo hekta 20 na Mbambabay hekta 27).
Tarehe 05 Novemba, 2022 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Thomas Elias Laban aliwakabidhi rasmi mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) hifadhi hiyo ili waiendeleze kwa kuongeza wanyama na kujenga mabanda ya kupumzikia.
Mpaka sasa jumla ya wanyamapori tisa wamewekwa ambao ni Swalapara watatu na Digidigi sita. Pamoja na wanyama hao, hifadhi hiyo ina wanyama wa asili kama Pimbi, Tumbiri, Fisimaji, Kenge, Nyoka, Mijusina Ndege wanaishi kandokando ya Ziwa (King fisher, Fish eagle, Commorant, Gunnet, Hammer cock).
Mchakato unaendelea wa kuongeza wanyama wengi na kulinda wanyama wa asili na Samaki wa mapambo waendelee kuongezeka. Kazi zinazoendelea kufanyika kwenye hifadhi hiyo ni:
Kufanya tathmini ya mazingira ya makazi ya wanyama (Habitat Assessment);
Mpango wa matumizi ya rasilimali zilizopo (Resource use Zone management Plan);
Tathmini ya athari ya mazingira (Environmental Impact Assessment);
Andiko la Kibiashara (Business Plan);
Kumalizia mchakato wa kuitanga hifadhi ya Mbambabay kwenye Gazeti la Serikali (Gazettment).
TAWA watachangia kuandaa kituo cha taarifa za vivutio vya utalii ambacho kitakusanya taarifa zote za vivutio vya mkoa wa Ruvuma ili wageni wanaoingia kupitia bandari ya Mbambabay waweze kupata taarifa kwa urahisi na sahihi zikiwepo za Samaki Adimu wa Mapambo wa Ziwa Nyasa.
6.1.5.8 Mazingira
6.1.5.8.1 Mkakati wa Kudhibiti Taka Ngumu
Hali ya Taka
Mkoa wa Ruvuma ni moja ya mikoa ambayo ina tatizo sugu la uzoaji takataka ngumu. Taka hizi ngumu zimezagaa sana hasa kwenye Miji Mikubwa ya Wilaya ikiongozwa na Mji wa Songea, Mbinga, Tunduru, Namtumbo na Mbambabay.
Kwa mji mkubwa wa Ruvuma Manispaa ya Songea huzalisha wastani wa tani 71.5 za taka kwa siku na uwezo wa Manispaa wa kuzoa taka ni tani 55 – 60 kwa siku sawa na asilimia 77 ya taka zote.
Aina ya takataka zinazozalishwa ni mabaki ya mazao ya chakula hasa kwenye masoko ya wakulima (kama Bombambili, Mfaranyaki na Mjimwema), pumba ngumu za mpunga hupatikana kwenye mashine za kukoboa mpunga (Mtaa wa Viwanda Mjini), Maranda ya mbao hupatikana wa wingi eneo la soko la mbao Mfaranyaki, mabaki ya vifungashio (Maboksi, mifuko ya nailoni na viroba), chupa za plastiki za vinywaji (Juisi, dawa), mabaki ya nguo chakavu na taulo (Pady) na vyuma chakavu ni vichache sana.
Matatizo ya kuongezeka kwa uchafu husababiswa na kuongezeka kwa idadi ya watu, kuongezeka Wafanyabiashara, Taasisi mbalimbali (Mashule, vyuo, magereza, mafesha). Sababu zingine ni uwezo mdogo wa Manispaa wa kuzoa takataka, mpaka sasa kuna magari matatu lakini linalofanya kazi ni moja tu na kijiko (Loader) cha kupakia takataka nacho kimekufa. Mradi wa kujenga dampo la kisasa Subira nao umesimama sababu ya ukosefu wa fedha, sababu zingine ni uelewa mdogo wa wananchi na kukosa hamasa ya swala la usafi wa mazingira kwa baadhi ya wananchi kutokushiriki siku maalum ya usafi wa mazingra ya kila mwezi na kutochangia gharama za usafi kwenye mitaa yao.
Mkakati wa Kupunguza Takataka
Kuanzisha vituo vya kuzalisha mboji (Composite)
Takataka za mabaki ya chakula (matunda, mboga za majani, mabua ya mahindi na majani ya mimea) huweza kutumika kutengeneza mboji ambayo inatumika kwenye bustani za mboga, maua na mashambani. Aina hii ya mbolea hukaa muda mrefu shambani na husaidia kutunza maji na kuboresha udongo;
Kituo cha mfano cha kuzalisha mboji cha eneo la bustani ya kilimo Msamala Miembeni bado hakijaanza kazi. Manispaa isimamie uanzishaji wa kituo hiki kwa kushirikiana na vikundi vya vijana au wakinamama.
Mashine za kutengeneza mkaa mbadala na majiko sanifu takataka zinazotokana na Maranda ya mbao (sawdust) na pumba ngumu za mpunga huweza kutumika kutengeneza mkaa mbadala (Briqutte and Pilets).
Kupitia sekta binafsi tayari kuna mashine mbili, lakina inayofanya kazi ni moja iliyopo Ruhira boys. Tatizo ni ukosefu wa soko kutokana na uelewa wa aina hii ya mkaa mbadala.
Maranda ya mbao huweza kutumika moja moja kwa kutumia majiko maalum sanifu ambayo hutumika hasa kwenye maeneo ya kitimoto. Taasisi zenye watu wengi (Mashule, vyuo, magereza, majeshi, mashirika ya dini) yahamasishwe kutumia mkaa huu mbadala au majiko maalum sanifu ya Maranda na pumba ngumu za mpunga. Teknolojia hii hutumika hata majumbani na maeneo ya kitimoto, chips na yanayotumia mkaa muda mrefu.
Mashine za Plastiki
Mashine hizi za kukusanya na kukatakata chupa za plastiki na kuzifunga pamoja kwa sasa hazipo kabisa hapa mjini Songea. Takataka hizi baadaye husafirishwa kwanye viwanda vya plastiki (Dar es Salaam au Tanga na Mbeta) na kutengenezwa bidhaa nyingine (recycle).
Usafirishaji taka ngumu kwa kushirikisha jamii, mkakati huu unashirikisha jamii ya mtaa mmoja kupanga kiwango cha mchango kwa ajili ya kupata fedha za kuajiri vibarua wa mtaani wa kuzoa taka na kukodi gari la kusafirisha taka hadi dampo. Mhusika mkuu ni Mwenyekiti wa Mtaa, wajumbe na wananchi kwa ujumla.
Kuchimba mashimo ya takataka
Mkakati huu unafaa zaidi kwenye maeneo ya pembezoni na yenye viwanja vikubwa (medium na low density plots). Kwa maeneo ya katikati ya miji au ya viwanja vidogo haiwezekani na badala yake maeneo hayo yanatakiwa kuwa na vifaa vya kukusanyia taka (mapipa, ndoo za plastiki).
Kuiongezea uwezo Halmashauri wa kuzoa taka
Manispaa ya Songea pamoja na Halmashauri zenye miji hazina magari ya kutosha ya kuzoa taka na yaliyopo ni machache na mabovu na yana kazi nyingi. Aidha, kuna upungufu mkubwa wa Mafuta ya magari unaotokana na bajeti ndogo.
Kwa kushirikisha wadau wengine au taasisi zingine zilizopo kwenye Halmashauri wanaweza wakasaidia kutoa magari ya kuzoa taka japo mara moja kwa mwezi hasa siku maalum ya usafi ya kila mwezi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.