6.1.4 SEKTA YA UVUVI
Katika sekta ya uvuvi, Mkoa unategemea kupata samaki kutoka ziwa Nyasa, mito, mabwawa ya asili na mabwawa ya kufugia samaki. Hata hivyo tija itokanayo na vyanzo hivyo vya samaki haitoshelezi mahitaji ya Mkoa ambayo ni zaidi ya tani 18,000 kwa mwaka, hivyo tunapata samaki kutoka nje ya Mkoa wastani wa tani 55 kwa mwezi, ukilinganisha na wastani wa mavuno ya samaki kwenye maji ya asili tani 151.5 kwa mwaka. Watalaamu wanaendelea kuhamasisha ufugaji wa samaki kwenye mabwawa ili kukidhi mahitaji ya walaji. Aidha, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 Julai hadi 2022 Septemba jumla ya wavuvi 7,635 walisajiliwa, pamoja na vikundi 38 vya wavuvi na vikundi 4 vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMUs) vilivyopo katika mialo ya Mbamba bay, Lituhi, Ndengele na Ng’ombo. Uzalishaji wa samaki katika Ziwa Nyasa ni wastani wa tani 8,411.4 kwa mwaka zenye thamani ya Tshs. 25, 234, 200,000.00.
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya wataalamu wa kada ya uvuvi 7 ambapo katika ngazi ya Mkoa ni mmoja (1) na nane(6) wako katika ngazi ya Halmashauri za wilaya.
Jedwali Na. 33: Wataalamu wa kada ya uvuvi kwa kila halmashauri
Halmashauri |
Wanaohitajika |
Waliopo |
Mapungufu |
Waliopo kwenye mpango wa kuajiriwa 2021/2022
|
Tunduru
|
12 |
1 |
11 |
0 |
Namtumbo
|
21 |
2 |
19 |
8 |
Mbinga DC
|
31 |
1 |
30 |
0 |
Nyasa
|
22 |
1 |
21 |
5 |
Songea DC
|
18 |
0 |
18 |
14 |
Madaba
|
9 |
1 |
8 |
0 |
Songea MC
|
5 |
0 |
5 |
5 |
Mbinga TC
|
14 |
0 |
14 |
1 |
Jumla
|
132 |
6 |
124 |
33 |
6.1.4.1 Uzalishaji wa Samaki Kwenye Mabwawa
Mkoa una jumla ya wafugaji wa samaki 4,170 wenye jumla ya mabwawa 6,602 yenye wastani wa uzalishaji wa tani 847.9 kwa mwaka.
Hata hivyo, Ufugaji wa samaki ni shughuli ambayo wananchi wengi wamekuwa wakiifanya katika kuongeza kipato na lishe katika jamii inayowazunguka. Kutokana na kutotosheleza kwa samaki wanaotoka kwenye vyanzo vya samaki vilivyopo kwenye Mkoa, wananchi wanaendelea kuhamasishwa kufuga samaki kwa tija katika mabwawa ili kuweza kukidhi mahitaji hayo kwa ajili ya chakula na kwa biashara pia.Ndani ya Mkoa kuna kituo kimoja (1) cha kuzalisha vifaranga bora vya samaki kwa ajili ya wafugaji,kituo hicho kipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ,Ruhila (RADC) kilichopo Manispaa ya Songea.
6.1.4.2 Fursa Katika Ufugaji wa Samaki
Halmashauri |
Idadi ya wafugaji |
Idadi ya mabwawa |
Uzalishaji (tani) |
Tunduru
|
315 |
463 |
3.90 |
Namtumbo
|
200 |
71 |
1.3 |
Songea M.C
|
955 |
937 |
7.1 |
Mbinga
|
954 |
1,293 |
8.4 |
Songea D.C
|
1,327 |
3,227 |
96.8 |
Nyasa
|
170 |
225 |
1.4 |
Mbinga Mji
|
215 |
310 |
1.2 |
Madaba
|
34 |
56 |
1.1 |
JUMLA
|
4,170 |
6,602 |
121.20 |
Chanzo: Halmashauri za Wilaya, Mji na Manispaa.
6.1.4.3 Matumizi ya Zana Bora Za Uvuvi.
Katika matumizi ya zana bora za uvuvi, jitihada zimewekwa ili kujenga uwezo kwa wavuvi kutambua madhara yatokanayo na matumizi ya zana haramu za uvuvi , utoaji wa elimu juu ya matumizi ya zana bora za kisasa za uvuvi zinazokubalika kisheria, kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kuhamasisha ufugaji bora wa kisasa na wenye tija. Pamoja na kuhamasisha uwanzishwaji wa vikundi vya ulinzi wa rasilimali za uvuvi BMUs (Beach Management Units) hasa katika mwambao wa ziwa Nyasa na mto Ruvuma ili rasilimali za uvuvi zitunzwe, zilindwe na ziwe endelevu. Aidha, ujenzi wa karakana ya kuunda boti za uvuvi za kisasa katika kituo cha Mbamba Bay umefikia hatua za mwisho za kuweka mashine.
6.1.4.4 Mikakati ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi.
Kutoa elimu endelevu ya uanzishaji wa vikundi vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi(BMUs) katika mwambao wa ziwa Nyasa.
Kuhimiza uanzishaji wa vituo vya uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki, ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (cage) katika ziwa na mabwawa ya asili ili kupata mavuno mengi ya samaki yatakayofaa kwa ajili ya viwanda.
Kukijengea uwezo kituo cha maendeleo ya ufugaji samaki Ruhila ili kiweze kuzalisha vifaranga bora na vya kutosha, kwa sasa kituo kina uwezo wa kuzalisha vifaranga 1,000,000.00 kwa mwaka ukilinganisha na mahitaji ya vifaranga 3,000,000 kwa mwaka.
Kila Halmashauri kuwa na kituo cha kuzalisha vifaranga bora vya samaki ambapo vituo hivyo vitatumika pia kama mashamba darasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.