Changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa vijiji vya Luhimbalilo,Naikes na Luhangano wilaya ni Namtumbo mkoani Ruvuma inakwenda kumalizika baada ya serikali kutekeleza mradi wa maji wa zaidi ya bilioni tatu .
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), imeanza kutekeleza awamu ya pili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Luhimbalilo-Naikes utakaowanufaisha wakazi zaidi ya 15,542 katika vijiji hivyo.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo Mhandisi Salome Method amesema mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya Trinity Manufacturing Service Ltd chini ya usimamizi wa RUWASA wilaya ya Namtumbo.
Amesema ,mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili na umetengewa zaidi ya Sh.bilioni 3.17 kati ya fedha hizo zaidi ya Sh.bilioni 1.7 zimetumika kutekeleza mradi awamu ya kwanza katika kijiji Luhimbalilo.
Amesema zaidi ya shilingi bilioni 1.46 zitatumika katika awamu ya pili ya mradi.
Kwa mujibu wa mhandisi huyo
,RUWASA wilaya ya Namtumbo imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Masuguru unaohudumia wakazi zaidi ya 3,264 kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 350.
Mkazi wa kijiji cha Luhimbalilo Said Juma,ameishukuru serikali kwa kujenga mradi huo kwa kuwa tangu kijiji hicho kilipoanzishwa miaka ya 70 hakijawahi kupata maji ya bomba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.