Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesajili wanachama milioni 12.4 kupitia mfumo wa kielektroniki hadi kufikia Aprili 2025, hatua inayokifanya kuwa chama chenye wanachama wengi zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, alitoa taarifa hiyo wakati wa mkutano na mamia ya wananchi wa Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni hitimisho la ziara yake mkoani humo.
Dkt. Nchimbi alisisitiza kuwa sera kuu za CCM zitaendelea kuzingatia maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Aidha, alieleza kuwa mafanikio yake katika kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi yanatokana na mchango wa wananchi wa Manispaa ya Songea waliompa nafasi ya kuwa Mbunge.
Katika Uwanja wa Majimaji, Dkt. Nchimbi aliwahutubia wananchi waliokusanyika kwa ajili ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ghorofa lenye fremu 50 za maduka, chini ya umiliki wa CCM Mkoa wa Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.