KINGERIKITI AMCOS YATOA ELIMU YA KAHAWA KWA WAKULIMA
Chama cha cha Ushirika cha Msingi cha Mazao na Masoko cha Kingerikiti (Amcos), kwa kushirikiana na Wafadhili wa chama hicho kutoka Nchini Marekani kupitia Shirika la USADF, Hivi karibuni Kimetoa Mafunzo kwa wakulima wa kahawa, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuzalisha na kuandaa kahawa bora ili kuongeza kipato kwa Mkulima.
Mafunzo hayo ya siku mbili, yametolewa katika Ofisi za Chama, zilizopo Katika Kijiji cha Kingerkiti, Kata ya Kingerikiti Wilaya ya Nyasa, na yametolewa na wakufunzi kutoka Shirika la Sturbucks yenye lengo la kuwafundisha wakulima namna ya kulima, kuitunza na kuandaa kahawa yenye Ubora ili kuifikisha Sokoni.
Akifungua Mafunzo hayo Afisa Ushirika wa Wilaya ya Nyasa Bw.Menance Ndomba alikipongeza chama hicho kwa kutoa mafunzo kwa wakulima yatakayowawezesha Wakulima, kukabiliana na wadudu waharibifu wa zao la kahawa ambalo pia ni zao la Kimkakati.
Aidha ametoa Wito kwa wanaushirika kushikamana, ili kuuendeleza Ushirika kwa kuwa ndiyo nguzo pekee kwa Wakulima wa Zao la Kahawa ambayo huwawezesha kuunganisha nguvu zao wakati wakuyafikisha mazao yao sokoni na kuhakikisha chama kinakwenda vizuri kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana hivyo wana kila sababu ya kushikamana.
“Ndugu zangu wanaushirika wa Chama Cha Msingi cha Mazao cha Kingerikiti, Nichukue Fursa hii kuwapongeza Viongozi wa Chama na wafadhili wa Chama hiki, USADF kwa kutoa mafunzo ambayo yanawajengea uwezo wakulima namna ya kulima, kupambana na wadudu waharibifu na kuiandaa kahawa bora itakayo washawishi wanunuzi, wanunue kahawa iliyokuwa na viwango vinavyokubalika na kwa bei nzuri, Aidha napenda kuwafahamisha rasmi kwamba kufuatia mafunzo haya mmeanzisha rasmi mchakato wakuyafikia masoko maalumu na kwa sasa tunajisajiri SOKO la CAFÉ Practice Nasema ahsante sana, Nitoe Wito kwa wanachama wa Chama hiki kushirikiana na kuendeleza Ushirika huu kwa kuwa Vyama vingi vikishapata mafanikio basi kutoelewana kunaanza kwa lengo la kuvuruga Ushirika, ” Alisema Ndomba.
Bw Ndomba aliyataja mafanikio yaliyopatikana Kingerikiti Amcos ni pamoja na kuwa na Mfuko wa Pembejeo wenye thamani ya milioni 38 ambao huwakopesha wakulima pembejeo na kulipa kipindi cha mavuno hali iliyosababisha kuongezeka kwa uzalishaji kutoka tani 10.3 mwaka 2017/2018 hadi kufikia tan 360.34 kwa Msimu wa mwaka 2019/2020. Mafanikio mengine nikukarabati ofisi na kununua vifaa vya ofisi, na kununua Mtambo wa kuchakata kahawa wenye thamani ya miliono 47.
Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Shirika la Sturbucks Bi Bahati Mlwilo amesema mafunzo yaliyotolewa kwa wakulima yamewajengea uwezo wa kulima kahawa ya Kisasa, kupambana na Wadudu wanaoharibu kahawa, namna ya kupambana na magonjwa ya kahawa.lakini pia wamejifunza namna ya kuiandaa na kuifiiksha kahawa yenye ubora na kuongeza kipato kwa kaya na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo Samweli Kinunda na Severine Mbunda, waliwapongeza wafadhili pamoja na viongozi wa Chama hicho, kwa kuandaa Mafunzo hayo ambayo yamewasaidia kutambua Changamoto katika zao la kahawa kwa kuwa awali walikuwa wanalima kienyeji na kupata mazao kidogo yasiyo na ubora, lakini kwa sasa watatumia mafunzo waliyopewa kuboresha na kuitunza kahawa na kuipeleka kiwandani ikiwa na ubora wa hali ya juu ili kujiongezea kipato.
Imeandikwa na Netho Credo
Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.