MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekabidhi hati ya Umiliki wa hekari 65 katika Manispa ya Songea kwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha .
Akizungumza mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema anayapongeza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Nayapongeza maono na nia ya dhati ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na amiri Jeshi Mkuu kwa kutoa fursa ya kuwezesha wananchi wafaidike katika Nyanja totauti”.
Ibuge amesema uwezeshaji unaenda kufanya Chuo cha Uhasibu Arusha tawi la Songea Ruvuma unawezeshwa kwa fedha nyingi ambazo ni za mkopo imempendeza Rais kupitia Wizara ya Elimu kujenga chuo kikubwa chenye uwezo wa kubeba wanafunzi zaidi ya 4000.
Ibuge ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea kuwa na mshikamano ili kuwa na maendeleo chanya ikiwa ni Mkoa uliobarikiwa na kuendelea kufunguka kibiashara.
Amesema uwepo wa chuo cha uhasibu Arusha tawi la Songea Ruvuma siyo fursa tu kwa vijana bali na kuongeza pato la Biashara katika Mkoa na wananchi wake.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dr. Mwaitete Cairo mara baada ya kukabidhiwa hati na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kutoa ardhi bure ili Chuo cha Uhasibu Arusha tawi la Songea Ruvuma kiweze kujengwa.
“Nawapongeza Viongozi wa Mkoa kwa kuona umuhimu na kutoa ardhi bure ili wananchi waweze kunufaika ni chachu ya maendeleo washikilie kwa nguvu zote”.
Makamu Mwenyekiti wa Bodo ya chuo cha Uhasibu Arusha Joseph Mwigune amesema wapo tayari kuwekeza kuanzia mwaka wa fedha ujao ili kuhakikisha huduma inamfikia mwananchi kwa ukaribu.
Mwigine amesema ni maagizo ya Mhe. Rais kuhakikisha huduma inawafika wananchi kwa ukaribu zaidi ikiwa kutoka Ruvuma hadi Dare es salaam na Arusha pana umbali mkubwa na gharama kuwa kubwa kwa mwanafunzi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde na Jakson Mbano
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Juni 15,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.