WILAYA ya Nyasa Mkoani Ruvuma imefanya uzinduzi wa siku ya upandaji miti kiwilaya katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa kupanda miti katika eneo la hospitali na pembezoni mwa barabara za Kilosa.
Mgeni rasmi wa uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri, ambaye alihamasisha wananchi na watumishi kupanda miti 400 katika eneo la hospitali na miti 300 pembezoni mwa barabara ya Kilosa.
Mhe. Magiri aliwataka wananchi kupanda miti na kuitunza ili Wilaya ya Nyasa iwe eneo la kitalii kwa kuwa imepangwa vizuri. Alisisitiza umuhimu wa kupanda miti kama sehemu ya juhudi za kutekeleza agizo la serikali la kupanda miti milioni 1.5.
Amewaonya wafugaji wa mifugo dhidi ya kuachia mifugokudhurura na kuharibu miti iliyopandwa, akibainisha kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka.
Naye Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Nyasa Elisha John,amesema wameandaa miche 30,000 ya miti kwa kila kata ili wananchi wapande na kuongeza kipato cha familia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.