• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HALI ya vitendo vya ukatili mkoani Ruvuma ni mbaya

Imewekwa kuanzia tarehe: December 10th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema hali ya vitendo vya ukatili katika Mkoa ni mbaya hivyo jamii yote inatakiwa kuwajibika ili kuhakikisha ukatili unakoma.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema, katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili na wiki ya watoa msaada wa kisheria  katika hafla iliyofanyika kimkoa katika viwanja wa Black Belt Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea,RC Thomas ameyataja matukio yaliyoripotiwa katika Jeshi la Polisi kwa kipindi cha miezi sita iliyopita mkoani Ruvuma yalikuwa 442.

Ameyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni kubaka matukio 24,shambulio la aibu matukio 45,mimba kwa wanafunzi matukio 49,shambulio la kudhuru mwali matukio 86 na kutumia lugha za matusi matukio 42.

“Katika jamii zetu ukatili umeshika kasi kubwa sana katika kipindi hiki,madhara ambayo yanasababishwa na vitendo vya ukatili ni kama vile kupoteza Maisha,ulemavu wa kudumu,msongo wa mawazo,umasikini mkubwa unaotokana na kushindwa kuwajibika na kuongezeka kwa Watoto wa mitaani’’,alisema RC Thomas.

Akizungumzia wiki ya watoa msaada wa kisheria katika Mkoa wa Ruvuma,RC Thomas amewataja moja ya kazi za Watoa Msaada wa Kisheria kuwa ni kusaidia mtu anapokutwa na hatari ya kufanyiwa ukatili na uonevu mwingine wowote.

Hata hivyo ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu  na kujenga jamii huru  katika shughuli za ujenzi wa Taifa.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Jeshi la Polisi nchini,katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba 2021,mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili ni Arusha,Tanga,Shinyanga,Mwanza na Mkoa wa kipolisi  wa Ilala (Dar es salaam).

Akitoa taarifa ya ukatili wa kijinsia na watoto kwenye maadhimisho hayo,Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira amezitaja aina tatu za ukatili kuwa ni ukatili wa kimwili ikiwemo vipigo na kujeruwi.

Mlimira ameitaja aina nyingine kuwa ni ukatili wa kingono ikiwemo ubakaji na ulawiti,ukatili wa kisaikolojia ikiwemo matusi na kejeli,ukatili wa kiuchumi ikiwemo kutelekeza familia na ukatili wa unyonyaji ikiwemo kutumikisha kwa kulipa ujira mdogo.

Hata hivyo amezitaja shughuli zilizofanyika  katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili,mkoani Ruvuma kuwa ni  kutoa elimu ya ukatili,kufanya mikutano katika Taasisi za kidini,kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na Kwenda kuwatembelea Watoto yatima.

Naye Mshauri Mkuu wa Masuala ya kijinsia na Mwakilishi wa Mradi wa Afya Yangu katika Mkoa wa Ruvuma John Toto amesema katika juhudi za kupambana na ukatili wa kijinsia mradi huo kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wameendesha mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma za afya 88 waliopata mafunzo ya kusaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2022 ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni Kila uhai una thamani: Tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Desemba 10,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.