MRADI wa Clabu ya wapinga Rushwa katika Halmashauri ya Mbinga imezinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Lt .Josephine Mwambashi.
Akisoma taarifa hiyo leo katika uzinduzi huo Mwanachama wa Clabu ya wapinga Rushwa kutoka shule ya wasichana Mbinga girls Imelda Kapinga amesema clabu hiyo inawanachama 161 na walimu walezi 2.
Hata hivyo amesema Clabu hiyo ya wapinga Rushwa ya Mbinga girls ilianzishwa mwaka 2017 ikiwa na wanachama 40 na kuimalika mwaka 2018 baada ya viongozi kutoka Wilaya ya Mbinga kutembelea mara kwa mara na kutoa Elimu.
“Hatimaye ilizinduliwa rasmi na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho tarehe 04/06/2018”.
Kapinga ameelezea mafanikio ya Clabu hiyo ya wapinga rushwa katika shule hiyo kuongeza wanachama mara dufu zaidi tangu kuanzishwa kwake,kusambaza elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa katika familia,utunzi wa nyimbo,ngonjera,mashairi,ngoma,maigizo na uchoraji wa katuni.
“Matarajio ya mradi wa clabu hiyo kuanzisha bustani ya matunda utakaowezesha kutembelea makundi ya watu wenye mahitaji maalumu na shughuli hizo zitazidi kutuunganisha wanachama katika mapambano dhidi ya rushwa”.
Kapinga amewapongeza walezi wa clabu ya Takukuru akiwemo Mkuu wa Shule na wanachama wote kwa ujumla na kaulimbiu inayosema kupambana na rushwa ni Jukumu langu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Josephine Mwambashi mara baada ya kuwasikia wanaclabu ya kupinga rushwa amesema wawe mstari wa mbele kutoa taarifa katika taasisi ya Takukuru mara baada ya kupata changamoto ya vitendo vya rushwa
Mwambashi amesema Clabu hizi zinaandaliwa sehemu mbalimbali katika shule za msingi na Sekondari na zinasaidia kutoa elimu kwa jamii na kuwaelimisha ndugu jamaa na marafiki ili kusaidia Serikali kutokomeza Rushwa.https://www.youtube.com/watch?v=e3PBMxMsdNY
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoa ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 4,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.