MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefunga mafunzo ya Sensa ngazi ya Mkoa kwa wakufunzi wa wilaya 257.
Mafunzo hayo ya Sensa yamefanyika katika ukumbi Chuo cha Ajuco Manispaa ya Songea, ambayo yalijumuhisha wakufunzi 257 ngazi ya Wilaya ambapo yanalenga kutoa elemu ya vitendo kwa wasimamizi 574 na makarani 5674 ambao watashiriki kwenye zoezi la Sensa .
RC Ibuge amewaimiza Wakufunzi hao waende kufanya kazi hiyo kwa kufuata miongozo na maelekezo walio pewa na wakufunzi wao wa kuu kwani watambue kuwa Serikali imewaamini kwa kuwapa jukumu la kusimamia zoezi la Sensa na Makazi. wao ni jeshi la Sensa kwa Mkoa wa Ruvuma.
“Tunarudia kuwaimiza kwasababu tunataka mkatende kile kinachohitajika tambueni ninyi ni Jeshi la Sensa kwa Mkoa wetu ”.
Amesema Wasiamazi wawe wazalendo na wakasimamie kwa weledi kazi kubwa iliopo mbele kwa heshima ya Taifa na mkoa.
Kwa upande wake maratibu wa Sensa Mkoa wa Ruvuma Mwantum Athuman ameeleza kuwa mafunzo hayo ya Sensa yametolewa kwa siku 21 kwa ngazi ya koa kwaajili ya wakufunzi wa Wilaya.
Amesema vitendea kazi kwaajili ya zoezi la Sensa vimepokelewa vya kutosha kwaajili ya kuanza kazi ifikapo Agosti 23,2022.
“Wakufunzi hawa wameiva na wapo tayari kwa kutoa mafunzo kwa Makarani ,wamefundishwa madodoso manne ” amesema Mwantum.
Hata ivyo Mkufunzi Mkuu wa mafunzo ya Sensa Mkoa wa Ruvuma Sospiter Jibuge amewapongeza wakufunzi hao kwa kujitoa na kujituma kwa mdaa wote wa mafunzo .
Amesema wakafanye kazi kwa kupita mafunzo waliyopata ndani ya siku 21 kwani kwa kutokufanya hivyo watasababisha Zoezi kuharibika .
Sensa ya watu na makazi inatalajiwa kufanyika J Agosti 23, 2022 Ikiwa Sensa ipo kikatiba na itasaidia Serikali kupanga mipango yake ya kimaendeleo, Sensa hufanyika baada ya miaka kumi na Sensa ya mwisho ilifanyika mwana 2012 .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde na Jackson Mbano
Kutoka Kitengo cha mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Julai 26,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.