MWENGE wa Uhuru unatarajia kuanza mbio zake mkoani Ruvuma kuanzia Juni 8 na kukamilisha mbio zake Juni 15,2024.
Kwa mujibu wa ratiba ya Mwenge wa Uhuru 2024,Mwenge wa Uhuru utapokewa mkoani Ruvuma ukitokea mkoani Mtwara Juni 8,2024 katika Kijiji cha Sautimoja wilayani Tunduru.
Kulingana na ratiba hiyo Mwenge wa Uhuru,Juni 8 utakimbizwa katika Halmashauri ya Tunduru,Juni 9 Namtumbo,Juni 10 Halmashauri ya Songea,Juni 11 Halmashauri ya Mbinga,Juni 12 Nyasa,Juni 13 Halmashauri ya Mbinga Mji,Juni 14 Songea Manispaa na Juni 15 Halmashauri ya Madaba.
Mwenge wa Uhuru unatarajia kukabidhiwa katika Kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe Juni 16,2024.
Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.