Katibu Tawala Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mtela Mwampamba, amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa afya katika zoezi la linaloendelea la umezeshwaji wa dawa za kinga tiba ya Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo Usubi na Minyoo ya tumbo.
Zoezi hilo hufanyika kila mwaka Kitaifa chini ya Wizara ya Afya kwa kushirikiana na RTI, ambapo kwa Manispaa ya Songea zoezi hilo limefanyika kuanzia Agosti 17 hadi 21 mwaka huu katika mitaa yote 95 ya manispaa hiyo kwa walengwa wenye umri wa miaka 5 na kuendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mwampamba amesema zoezi hilo limefanyika kwa kaya 76,843 zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.