Akifungua kikao, mwenyekiti wa Baraza la biashara ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe . Cosmas Nshenye amewataka waataalamu wa kilimo na maafisa ugani kufanya tafiti na kupata majibu ya ni ainagani ya udogo na utafaa katika mazao yapi ili kuleta wigo mpana kwa wakulima na kuwa na mazao mbadala katika uwekezaji na sio kilimo cha mahidi pekee.
Atahivyo wataalam hawo wamesema uzalishaji mkubwa usitegemee beiyake kuwa juu hivyo wakulima wachukulie changamoto hiyo kama fulsa kwa kuanzisha viwanda ili kuongeza thamani ya mazao hayo .na kuwa taka mafiasa masoko kutafuta masoko ndani na nje ya nchi
Akizungumzia kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Kiamili, ambako ni Makao Makuu ya Halmashauri, Mkurugenzi Mnwele amesema kwa sasa Halmashauri hiyo inatekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi na ujenzi wa stendi ya mabasi na kwamba anatoa hamasa na kuwakaribisha wadau wa uwekezaji kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya eneo hilo, akitolea mfano kuwekeza kwenye ujenzi wa vibanda zaidi ya 200 vya biashara vitakavyojengwa kuzunguka eneo la stendi kwa kuingia ubia na Halmashauri hiyo.
Kikao cha Baraza la Biashara Wilayani Mbinga kimefanyika na kuongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Cosmas Nshenye na kuhudhuriwa na viongozi, wafanya biashara na wadau wa biashara kutoka Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Mbinga ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Na Makangury
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.