Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ikishirikiana na wadau wa sekta ya afya inawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Ruvuma katika Uwanja wa Majimaji kuanzia Novemba 24,2024 na kilele chake ni Desemba Mosi mwaka huu..
Katika wiki ya maadhimisho hayo, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na wadau wa afya itatoa huduma mbalimbali za afya ikiwemo;
Huduma za ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa Virusi vya UKIMWI, Uchangiaji wa Damu Salama,Kupima Kisukari na Shinikizo la Juu la Damu,Chanjo ya Homa ya ini na Kutoa elimu na msaada wa masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Watoto
Mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Chagua Njia Sahihi Tokomeza UKIMWI". Shime wana Ruvuma, jambo hili ni letu sote, tujitokeze na tushiriki kikamilifu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.