Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uwekezaji Mkoa wa Ruvuma Jeremiah Sendoro amewataka wataalamu Manispaa ya Songea kuhakikisha wanendelea kufuatilia na kusimamia kwa weledi miradi yote inayoendelea kujengwa ili iweze kukamilika kwa wakati.
Miongongoni mwa miradi iliyotembelewa na timu ya wataalamu kutoka Sekretarieti ya MKoa wa Ruvuma ni pamoja na ujenzi wa madarasa saba katika Sekondari ya Mdandamo inayojengwa kwa gharama ya Mil. 170.5, ukamilishaji wa Hospitali ya Manispaa ya Songea inayojengwa kwa gharama ya mil. 800 fedha kutoka Serikali kuu.
Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa manne na matundu 10 ya vyoo Sekondari ya Msamala inayojengwa kwa Mil. 115.5, ukamilishaji wa matundu ya vyoo Shule ya Msingi Shikizi Mkuzo inayojengwa kwa Mil. 10 fedha za mapato ya ndani, Ujenzi wa madarasa nane shule ya Sekondari Siri inayojengwa kwa Mil. 192 na ujenzi wa madarasa 10 shule ya Sekondari Londoni inayojengwa kwa Mil. 242.5 .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.