MBUNGE wa Jimbo la Madaba MheshimiwaJoseph Mhagama ametembelea Hospitali ya Hal,mashauri ya Madaba iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi Bilioni tatu ambayo tayari imeanza kutoa huduma.
Mhagama amesema atahakikisha Jimbo la Madaba linasonga mbele katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali ambayo inaletwa Madaba.
Mbunge amewashukuru Viongozi wa chama cha Mapinduzi kwa kuonesha ushirikiano pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Madaba kwa kusimamia na kutekelleza miradi mbalimbali ya maendeleo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Mheshimiwa Teofanes Mlelwa amempongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kuhakikisha Madaba inakuwa na Hospitali ya Wilaya na vituo vya Afya vitatu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.