• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MFUMO wa stakabadhi ghalani wawaingizia wakulima Ruvuma bilioni 87

Imewekwa kuanzia tarehe: May 30th, 2023

WAKULIMA mkoani Ruvuma wameweza kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 87 baada ya kuuza mazao ya ufuta,soya,mbaazi,korosho na kahawa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika kipindi cha mwaka 2022/2023.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas katika hotuba yake iliyosomwa na Mwakilishi wake Mhe.Kapenjama Ndile kwenye jukwaa la maendeleo ya ushirika Mkoa wa Ruvuma lililofanyika katika ukumbi wa Chandamali mjini Songea.

Kanali Thomas amesema kati ya fedha hizo  wakulima waliuza ufuta tani 7,970 zilizowaingizia shilingi bilioni 5.97 na mbaazi tani 6,647 zilizowaingizia shilingi bilioni 5.21.

Amebainisha zaidi kuwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima mkoani Ruvuma,waliuza korosho tani 15,315 zilizowaingizia shilingi bilioni 23.9 na kwamba waliuza kahawa tani 4,856 zilizowaingizia wakulima shilingi bilioni 31.61.

“Natoa wito kwa Halmashauri zote na viongozi katika ngazi zote tuwe na mpango kabambe wa kusimamia mfumo wa stakabadhi ya ghala na wakulima kujiunga na kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi za vyama vya ushirika’’,alisisitiza Kanali Thomas.

Amewatahadharisha wadau wa ushirika kutowaruhusu wanaotaka kupindisha sheria  kwa sababu wataua ushirika na kwamba wasiruhusiwe wafanyabiashara au mtu yeyote anayetaka kukwamisha mfumo wa stakabadhi ghalani.

Amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 itahakikisha dhana ya ushirika wa hiari inajengwa na kusimamiwa na sheria ili kuwalinda na kuwanufaisha wanaushirika hivyo kuchangia ustawi wa ushirika na Taifa kwa ujumla.

Awali  Stella Msengi akisoma risala ya wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika katika Jukwaa la Ushirika wa Mkoa wa Ruvuma, amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufanyia kazi changamoto mbalimbali zilizokuwa zinaikabili jamii kupitia vyama vya ushirika.

Amesema Mkoa wa Ruvuma hadi sasa una jumla ya vyama vya ushirika 293  kati ya hivyo vyama vya ushirika vya akiba na mikopo ni 62,vyama vya  ushirika wa masoko ya mazao 222 vyama vikuu vya ushirika vitatu na vyama vya ushirika vinginevyo sita.

Risala hiyo imeyataja baadhi ya mafanikio ya vyama vya ushirika katika Mkoa wa Ruvuma kuwa ni kuratibu upatikanaji wa pembejeo,kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao na bidhaa,kusimamia masoko ya mazao na bidhaa na kusimamia matumizi ya vipimo sahihi vya mauzo ya mazao ya wakulima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Ruvuma Justine Welo  amesema ushirika ni Taasisi ambayo inapigwa vita na watu wanaotaka kuwanyonya wakulima kwa kuwa ushirika unahusika na mazao ya kimkakati kama kahawa na korosho.

Amesisitiza kuwa katika kipindi cha mavuno kumekuwa na vita ya kugombea mazao hayo hivyo ametoa rai kwa serikali kuweka sheria ya Ushirika  kusimamia mazao ya kimkakati.

Kaulimbiu ya mwaka huu ya Jukwaa la Ushirika ni Ushirika kwa maendeleo endelevu.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Mei 30,2023

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.