Wakulima wa zao la ufuta na soya wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamenufaika na mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kupata zaidi ya shilingi bilioni 4 baada ya kuuza mazao hayo kupitia mfumo huo kwa msimu wa kilimo wa mwaka 201/2020.
Afisa Ushirika wa Halmashauri hiyo Bw Shekiel Massawe amesema katika kipindi hicho cha msimu wa kilimo cha mwaka 2019/2020, wakulima wamefanikiwa kuuza jumla ya kilogramu 2,378,172 za ufuta na kilogramu 100,774 za zao la soya.
Massawe amesema katika mauzo hayo Halmashauri imepata jumla ya shilingi milioni 259,462,700 kutokana ushuru wa kuuza mazao kwanjia mfumo huo.
“Stakabadhi ghalani ni mkombozi kwa mkulima kwasababu unampa mkulima uhakika wa soko na bei”,alisema Massawe.
Massawe amesema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mkombozi kwa wakulima kwa sababu unamsaidia mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya uhakika na kumwongezea kipato,upatikanaji wa soko,na kwamba wanalipwa kwa wakati ndani ya siku mbili baada mnada kufanyika.
Ameongeza kwa kusema kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani umetoa uwigo mpana kwa mkulima kuuza mazao yake tofauti na awali kabla ya mfumo, na kwamba baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wakiwanyonya wakulima kwa kuwapangia bei wanazo taka wao.
Amesema Mfumo wa stakabadhi ghalani ulianza mwaka kwa lengo la kuwasidia wakulima kuuza mazao yao na upatikanaji wa uhakika wa soko na kwamba katika kipindi cha kunzia Mei 4 hadi Agosti 5 mwaka huu jumla ya minada tisa imefanyika.
Mazao yaliyopendekezwa kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ni ufuta, soya na mbaazi.Hata hivyo amesema kwa msimu wa kilimo wa 2019/ 2020 mbaazi hazikuuzwa kwa sababu wakulima hawakufikisha zao hilo mnadani.
Imendikwa na Jackline Clavery
Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya Songea
Septemba 14,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.