MrajisI wa vyama vya Ushirika Nchini Dkt Benson Ndiege amewataka Viongozi,wanachama wa Ushirika na wakulima kuja kujifunza soko la mfumo wa stakabadhi ghalnani mkoani Ruvuma kwasababu Mkoa umefanikiwa katika kusimamia na kuendesha soko hilo.
Dkt Ndiege ametoa kauri hiyo wakati akishuhudia ufunguzi wa soko la pili la mnada wa kitaifa wa mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni.
Dkt Ndiege amesema mkoa wa Ruvuma umefanikiwa katika kuelimisha wakulima na kuwaunganisha pamoja katika soko la mfumo wa stakabadhi ghalani,hivyo amewataka Viongozi,wanachama wa Ushirika na wakulima kufika Ruvuma kujifunza juu ya mfumo huo.
“Nyie Songea au Ruvuma ni mfano mzuri kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani nawapongeza”,amesema Dkt Ndiege.
Amesema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo shirikishi kwa wakulima na wafanyabiashara ambao unatoa fursa kwa wakulima kukusanya na kuuza mazao yao kwa pamoja na kutatua changamoto za ukosefu wa soko la uhakika vilevile humpunguzia mnunuzi gharama za ufuatiliaji na uhakika wa kupata mazao yenye ubora.
Amewataka wafanyabiashara kujali maslahi ya wakulima kwa kununua mazao hayo kwa bei ambayo hai mkatishi tamaa mkulima katika kuendelea kuzalisha zao hilo ambalo uzalishaji wake ni mgumu ukilinganisha na mazao mengine.
Kwa upande wake Afisa shughuli wa chama kikuu cha Ushirika cha SONAMCU Zamakanaly Komba amesema katika soko la mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima ndiyo mtaji katika kuendesha soko hilo na wanamamlaka ya kukubali au kukata kuuza mazao yao endapo bei inyotajwa kutokuwa na maslahi kwao.
Imeandikwa na Jakline Moyp
Afisa Habari Halmashauri ya Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.