MKOA wa Ruvuma umeweka mikakati ya kuendeleza sekta ya uvuvi wa Samaki ili kuhakikisha Zao hilo linakidhi mahitaji ya wananchi.
Akizungumza afisa Uvuvi Mkoa wa Ruvuma Amuli Bazil ofisini kwake amesema mikakati hiyo ikiwemo kuhimiza matumizi ya zana bora za uvuvi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ambapo hadi kufikia Septemba 2022, zaidi ya wavuvi 5,380 na wafugaji 4,159 na wadau 279 wamefundishwa njia za uvuvi wa Samaki na utunzaji wa mazingira.
Bazil amesema njia bora ya kuendelea uvuvi wa samaki ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya uvuvi hasa mialo (Land stations), na katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
“Elimu endelevu ya uanzishaji wa vikundi vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMUs) katika mwambao wa Ziwa Nyasa”.
Hata hivyo amesema wamejipanga kuhimiza uanzishaji wa uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki,ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (cage) katika ziwa na mabwawa ya asili ili kupata mavuno mengi ya samaki yatakayofaa kwaajili ya viwanda.
Amesema mkakati wa kukijenga kituo cha maendeleo ya ufugaji samaki Ruhila ili kiweze kuzalisha vifaranga bora na vya kutosha,kwa sasa kituo kinauwezo wa kuzalisha vifaranga 1,000,000 kwa mwaka ukilinganisha na mahitaji 3,000,000 kwa mwaka.
“Halmashauri iwe na kituo cha kuzalisha vifaranga bora vya samaki ambapo vituo hivyo vitafanyika kama shamba darasa “.
Amesema Ujenzi wa Soko la samaki Mbamba bay Wilaya ya Nyasa upo katika hatua za mwisho ili liweze kutumika pamoja na ujenzi wa boti 6 za kisasa za Halmashauri bado unaendelea.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Octoba 19,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.