• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKURUGENZI Manispaa ya Songea akabidhiwa mwongozo wa mfumo wa anwani za makazi

Imewekwa kuanzia tarehe: May 17th, 2021

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akimkabidhi Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo wakati Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikitambulisha programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile Application) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwa Wakurugenzi wa halmashauri na Makatibu Tawala wa mikoa katika Mkutano wa 11 wa TOA uliofanyika jijini, Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula na timu yake ya wataalamu wametoa wasilisho la programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile App) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi  pamoja na hatua iliyofikiwa ya usimikaji wa Mfumo huo nchini kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mkutano wa 11 wa Maboresho ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TOA).

 

Akizungumza katika mkutano huo jijini Dodoma, Dkt. Chaula amesema kuwa Wizara hiyo inatekeleza ujenzi na usimikaji wa Mfumo huo kupitia Halmashauri zote nchini ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/21 halmashauri 13 ziliingizwa kwenye mpango wa kusimikwa mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi.

 

Ameongeza kuwa mpango wa Wizara hiyo ni nyumba zote nchini ziwe na Anwani za Makazi ifikapo June 2022 na kuzipongeza halmashauri za mji wa Bukoba na Jiji la Mwanza kwa kuwa vinara wa utekelezaji wa Mfumo huo

 

“Ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya Mfumo huu Wizara imetengeneza programu tumizi ya simu ya mkononi (mobile application) ambayo itawezesha kutambua na kuonesha nyumba ilipo au popote mwananchi anapotaka kwenda na pia utarahisisha shughuli za biashara”, alizungumza Dkt. Chaula

 

Akizungumzia mwongozo wa utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi,  Dkt. Chaula amesema kuwa mwongozo huo umefanyiwa maboresho na utagawanywa kwa wadau kwa sababu utekelezaji wake unahusisha Wizara zaidi ya moja ikiwemo TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu kama Serikali na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiwa kama sekretarieti.

 

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Wizara hiyo ameizungumzia programu tumizi ya Mfumo huo kuwa na manufaa mengi kiuchumi na kijamii hasa katika dhana nzima ya  uchumi wa kidijitali ambapo mfumo huo utarahisisha shughuli za kiuchumi kuweza kufanyika kidijitali.

 

Ameongeza kuwa chimbuko la mfumo huo ni Sera ya Taifa ya Posta inayoelekeza kuwa na Anwani ya Makazi ili kuweza kufikishiwa huduma mahali mwananchi alipo na kuongeza manufaa ya kijamii, kiuchumi na pia kimataifa ambapo nchi ya Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Posta Afrika.

 

Naye Mhandisi Jampyon Mbugi wa Wizara hiyo amezungumza na wajumbe wa Mkutano huo na kuwaomba kila mmoja kutimiza wajibu wake na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha zoezi zima la usimikaji wa majina ya barabara, mitaa na namba za nyumba pamoja na  ukusanyaji wa taarifa za makazi.

 

Aidha, wataalamu wa programu tumizi ya mfumo huo waliitambulisha program hiyo kwa wajumbe wa kikao hicho na kuonesha namna ya kuingia katika program hiyo na jinsi ya kuitumia ambapo inaonesha njia na barabara ya kupita mpaka kufika mahali ambapo mtumiaji anataka kufika.



Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.