Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi katika Manispaa hiyo Bashir Muhoja amewashukuru waandishi wa habari kwa mchango wao mkubwa wa kupasha habari tangu kwa kuanza zoezi la uandikishaji na katika kuhakikisha kuwa upigaji kura unafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia taratibu za uchaguzi.
Mshikamano na ushirikiano wa waandishi wa habari umeonekana kuwa na umuhimu mkubwa katika kutoa taarifa za haraka na za kuaminika kwa wananchi, hivyo kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unakuwa wazi kwa umma.
“Mpaka sasa naweza nikasema kwanza niwashukuru sana ninyi waandishi wa Habari kwa msaada mkubwa mmetupa tangu tumeanza zoezi hili kupasha habari mbalimbali kwa hatua mbalimbali ikiwa ni hatua za uandikishaji ambapo mlitusaidia sana na kufanikiwa kwenye Mkoa wetu tuliongoza Manispaa kwa kuandikisha wananchi 186,000 ambayo kwa kweli ni idadi kubwa ikiwa ni asilimia 106 ya makadirio ambayo tulikuwa tumekadiria” amesema Muhoja.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.