KULIA ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Vinsent Kayombo akizungumza na wataalam zaidi ya 280 kutoka mikoa ya Ruvuma,Njombe na Iringa wanaopata mafunzo ya Mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) mjini Iringa.Ameziagiza Timu za utekelezaji miradi ya BOOST kuhakikisha utekelezaji wa miradi uendane na ubora na thamani ya fedha.
Kupitia mradi wa BOOST wenye lengo la kuboresha Elimu ya Awali na Msingi,serikali inatarajia kutumia shilingi trilioni 1.15 kutekeleza mradi huu kwa miaka mitano ambapo madarasa 12,000 na shule salama 6,000 zinatarajiwa kujengwa nchini .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.