Katika kijiji cha Misiaji, Kata ya Marumba wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, umeibuka ushuhuda wa kipekee.
Mlima mkubwa na mrefu wa Chingoli umegundulika kuwa na mapango yenye udongo wa kipekee, wenye rutuba ya asili inayochochea ustawi wa mazao kwa kiwango cha juu kabisa.
Wananchi wa vijiji 11 vinavyounda Jumuiya ya Uhifadhi wa Jamii (WMA) ya Chingoli, wameeleza kuwa wamekuwa wakitumia udongo huo kwenye mashamba yao, na matokeo yake ni mavuno mengi, bora na yenye afya nzuri ya mazao. Mbolea ya asili kutoka mlima huo imekuwa hazina isiyo na kifani kwa wakulima wa maeneo hayo.
Wanakijiji hao sasa wanaomba Serikali kutembelea mlima huo ili kufanya uchunguzi wa kitaalamu, kwa lengo la kuvutia uwekezaji wa kiwanda cha mbolea ambacho kitaongeza ajira, kipato cha wananchi na mapato ya serikali.
Mbali na hazina ya udongo wenye rutuba, Chingoli pia ni kivutio cha kipekee cha utalii – ikiwa na mandhari ya kuvutia, wanyamapori kama tembo na nyati, pamoja na mapango ya asili yanayoweza kugeuzwa kuwa vivutio vya kipekee kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.