Kupitia makubaliano rasmi yaliyosainiwa Novemba 2023, CT Limited imeingia ubia na WMA tano: Nalika na Chingoli (Tunduru), pamoja na Kisungule, Kimbanda, na Mbarang’andu (Namtumbo), zenye jumla ya eneo la zaidi ya hekta 856,600—sawa na kilomita za mraba 8,566.
Licha ya kutofikia hatua ya kuuza vyeti vya kaboni, hatua muhimu tayari zimechukuliwa: wataalamu kutoka NCMC wameshakamilisha vipimo vya awali vya kaboni katika misitu, hatua inayofungua milango ya uthibitishaji wa mradi katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
UWEKEZAJI WA BILIONI 1.2 KWA MANUFAA YA MAZINGIRA NA JAMII
Hadi sasa, zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 zimeshawekezwa na CT Limited. Kati ya fedha hizo,Milioni 606 zimeelekezwa kwenye kulinda na kusimamia maliasili na Milioni 663 zimetumika kuimarisha huduma za jamii kama vile,Ujenzi wa madarasa, zahanati na nyumba za walimu,Ununuzi wa madawati kwa shule,Huduma za bima ya afya na Utoaji wa chakula mashuleni.
Mpango huu unaifanya biashara ya kaboni isiwe tu njia ya kuhifadhi mazingira, bali pia daraja la kuinua maisha ya wananchi wa vijijini kwa huduma bora na miundombinu ya maendeleo.
CT Limited imelenga Kukamilisha maandiko ya mradi na kuyawasilisha kwa mamlaka husika mwaka 2025,Kufanikisha uthibitishaji rasmi na kuanza kuuza vyeti vya kaboni ifikapo 2025/2026 na Kupanua mradi kwa kushirikiana na jumuiya mpya kama Ifinga na vijiji 12 vya Tunduru.
RUVUMA YAWEKA ALAMA KATIKA RAMANI YA MAENDELEO ENDELEVU
Mradi huu wa kaboni ni zaidi ya biashara—ni dira ya maendeleo jumuishi inayojumuisha uhifadhi, elimu, afya, na kipato mbadala. Ikiwa mfano huu utatekelezwa kikamilifu, Ruvuma inaweza kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika katika kuoanisha mazingira na maendeleo.
#CarbonTanzania #KaboniRuvuma #GreenEconomy #UhifadhiTanzania #WMA #MaendeleoVijijini #ClimateAction #CarbonCredits #RuvumaYetu #MazingiraBoraMaishaBora
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.