Dc Julius Mtatiro amewataka watumishi wa umma na watumishi wote ambao wameteuliwa na Mh, Rais amewataka wasijisahau katika utumishi wa umma uku akiwataka wafanye kazi kwa bidii ili ata siku wakitoka alama ya kazi zuri waliofanya itaendelea kuwepo katika wilaya yaTunduru.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mtatiro amewambia wageni ambao wameshiriki futari ambayo aliandaa amewaeleza kuwa Halmashauri adi sasa inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo tayari Halmashauri imetenga fedha milioni 200 kwajili ya ujenzi wa Zahanati 5.
Pia kwa upande wa wageni ambao walishiriki katika futari hiyo walimshukuru sana mkuu wa wilaya kwa kuandaa futari hiyo uku wakihaidi kuwa Waislamu na wananchi wote kwa ujumla katika wilaya ya Tunduru watashirikina na serikali pale watakapo takiwa kutoa ushirikiano wao.
Mwisho Mkuu wa wilaya aliwashukuru sana viongozi wa dini na Serikali pamoja na Wananchi wote ambao walikubali kushiriki mwaliko wake huo wa kufuturisha uku akimuomba mwenyezi mungu awalinde watu wote walioudhuria tukio hilo la kufuturu na kuwapatia afya njema pale wanapo rejea majumbani kwao wanapo toka katika viwanja hivyo vya ikulu ndogo Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.