Mwenge wa Uhuru 2025 umeikubali miradi yote tisa yenye thamani ya shilingi bilioni1.6 iliyopitiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji safi na salama katika gereza la kilimo Kitai ambao umefunguliwa na Mwenge wa Uhuru ukiwa na uwezo wa kuhudumia wakazi1468.
Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ,Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mbinga Mashaka Sinkala alisema mradi huo umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 400 kutoka serikali kuu.
Mradi mwingine uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya Ya Mbinga ni mradi wa jengo la huduma ya mionzi katika hospitali ya Mtakatifu Gaudensia iliyopo Mkako.
Akitoa taarifa ya mradi huo ,Mkurugenzi wa Hospitali ya Mtakatifu Gaudensia Dr.Thadei Kinyero alisema jengo hilo linatoa huduma na ambazo alizitaja kuwa ni huduma ya mionzi,kipimo cha kutambua hali ya moyo,radiolojia na kipimo cha umeme wa moyo na kwamba hadi sasa jengo hilo limetoa limetoa huduma ya wagonjwa 4049.
Hata hivyo amesema mradi huo wa jengo la radiolojia umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 435.
Mradi mwingine ambao umepitiwa na mwenge wa Uhuru ni mradi wa uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji katika shule ya msingi Kiamili kijiji cha Kigonsera ambapo wanafunzi wameweza kuchimba mabwawa manne kwa gharama ya shilingi 700,000.
Mwenge wa Uhuru pi umetembelea mradi wa uwekezaji katika shamba la miti la Mbuji lenye ukubwa wa hekari 65.7 zenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 29.
Mwenge wa Uhuru pia umepita katika mradi wa ,mabweni mawili katika shule ya sekondari Mbuji ambapo serikali imetoa Zaidi ya shilingi milioni 275 kutekeleza mradi huo.
Miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni mradi wa klabu ya wapinga rushwa na shamba la kahawa la mkulima binfasi Herbahat Raphael lililopo katika kijiji cha Nyoni.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati anakagua miradi hiyo,Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025 Ndugu Ismalil Ali Ussi amewapongeza viongozi katika ngazi zote na wananchi wilayani Mbinga kwa kusimamia utekeleza wa miradi hiyo ambayo inakwenda kuleta manufaa makubwa kwa wananchi.
Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa anatoa fedha nyingi zikiwemo za maji,afya,barabara na elimu ili kuhakikisha wananchi wanatatuliwa changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Ametoa rai kwa wananchi wote waliojiandikisha kuhakikisha wanajitokeza kwenye uchaguzi mkuu kupiga kura mwezi Oktoba ili kuwachagua madiwani,wabunge na Rais.
Mwenge wa Uhuru upo mkoani Ruvuma ambapo unatembelea miradi katika Halmashauri zote nane na utakabidhiwa mkoani Mtwara Mei 17 mwaka huu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.