MRADI wa Madarasa mawili ya shule ya Msingi Mtyangimbole umezinduliwa na kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Lt Josephine Mwambashi na ametembelea mradi wa lishe pamoja na kukagua banda la Malaria.
Ujenzi wa Madarasa hayo umegharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 40 kutoka Serikali kuu na nguvu kazi za Wananchi shilingi milioni 5.5, na kubaki shilingi zaidi ya milioni 4 na kutumika kukarabati madarasa mengine.
Mara baada ya kuzinduliwa kwa Madarasa hayo Kiongozi huyo amesema umuhimu wa madarasa hayo yataongeza ari ya wanafunzi kupata hamasa ya kujisomea kwa usahihi na amewaagiza wanafunzi kutumia vizuri na wengine wajao watumie.
Mwambashi ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kusimamia mradi huo kwa viwango vinavyotakiwa na kuhakikisha kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 4 kinabaki na kutumia kukarabati madarasa mengine ya shule hiyo.
“Gharama za mradi huo tulipokea fedha kutoka Serikali kuu milioni 40 na nguvu ya wananchi ni milioni 5.5, mradi huo umejengwa kwa kutumia force account”.alisema Mkurugenzi wa Halmashauri.
Wakati huo huo katika kuboresha afya ya wananchi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed ameuongea mradi wa lishe ikiwemo siku ya afya ya Lishe ya kijiji cha Likalangilo,ambayo ni mpango jumuishi ya kuboresha upatikanaji wa Afya kwa jamii na kuwajengea uwezo wa kutambua jinsi ya kuzuia utapiamlo.
Amesema Wilaya ya Songea inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu lishe bora na umuhimu wa Lishe bora katika familia na jamii kwa ujumla kwa kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo klini ya kila mwezi kwa wazazi na walezi wa watoto chini ya miaka mitano,siku za afya za Lishe zinazofanyika kila robo ya mwaka.
Hata hivyo ameelezea wananchi wa Halmashauri ya Mdaba wanavyoelewa umuhimu wa Lishe na wanaendelea kuwafahamisha juu ya umuhimu wa lishe bora na athali zitokanazo na lishe duni na madhara ya utapia mlo.
Vile vile Mkurugenzi kwa upande wa Malaria amesema Ugonjwa wa malaria ni miongoni mwa Magonjwa 10 yanayoongoza kuhatarisha maisha ya jamii katika Wilaya ya Songea.
“Hali ya maambukizi imepungua kwa wastani wa kutoka asilimia 11.5 mwaka 2019 na kufikia asilimia 8.1 mwaka 2021,hii ni kutokana na hatua mbalimbali ambazo zilikuwa zikichukuliwa na idara ya afya”.
Ameelezea utekelezaji wa kuhakikisha Ugonjwa huo unadhibitiwa kwa matibabu kwa kutumia kanuni na miongozo ya Wizara ya Afya kwa walewanaobainika wameambukizwa Uganjwa kwa wajawazito wanaoanza kliniki na watoto chini ya miaka mitano.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari Ruvuma
Septemba 6,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.