WAKULIMA wa Halmashauri ya Wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma wameishukuru na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt, Samia Suhulu Hassan kwa kuboresha uuzaji wa mazao kupitia Mfumo wa stakabadhi ghalani.
Hayo wamesema katika mnada wa ununuzi wa zao la ufuta uliofanyika katika kata ya Lisimonji wilayani umo ambapo Kampuni ya Kinasoru East Africa (T) Ltd imenunua kilo moja ya ufuta kwa shilingi 4105 hivyo kuzishinda Kampuni 17 zilizokuwa zinashindana kwenye mnada huo.
“Tunaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais Mama Samia kwa kutuletea mfumo wa stakabadhi ghalani sisi leo tumepata bei ya kuuza ufuta kilo moja kwa bei ya shilingi 4105 tumefurahia tunaiomba Serikali kuwa mfumo huu uendelee na kutakuwa tunazalisha ufuta mwingi.”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.