Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Leo imeanza kutoa mafunzo ya siku tatu ya Mpango wa usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano (05), kwa washiriki 121 kutoka Kata zote na Vituo vyote 35 vya kutolea huduma za afya, ili kuwajengea uwezo washiriki namna ya kuwasajili watoto hao.
Mafunzo hayo ni ya siku tatu, yanayofanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba ulioko Katika Kata ya Mbamba-bay Wilayani hapa, yanatolewa na Serikali kupitia Wakala wa Usajili,Ufilisi na Uthamini (RITA) .
Akifungua mafunzo Hayo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba aliwataka washiriki hao kuzingatia Mafunzo,maadili ya kazi wanayoenda kuifanya kwa kuwa, wanaenda kuwasajili watoto ambao ni Raia wa Tanzania na kuwataka kuongeza umakini kwa kuwa wilaya ya Nyasa Inapakana na Nchi mbili ya Malawi na Msumbiji ili wasiweze kuwasajili watoto wasio raia wa Tanzania.
Bi chilumba aliongeza kuwa zoezi hili la Usajili wa watoto, waliokuwa chini ya umri wa miaka mitano ni kubwa na linatakiwa kutekelezwa kwa umakini na kufikia Lengo la kusajili kwa asilimia mia moja pamoja na kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kuwapatia watoto wao Vyeti vya kuzaliwa, kwa kuwa wato wengi hawana vyeti hivyo licha ya kuwa ni muhimu sana.
Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi la Usajili Wilaya ya Nyasa,Bi Imelda Mlugo amesema Wilaya ya Nyasa inatarajia kusajili watoto (27,669) na jumla ya vituo vya usajili vitakuwa (35) na idadi ya washiriki wa mafunzo hayo ni 121 kutoka Kata 20 za Wilayani Hapa.
Alitoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kujitokeza kwa wingi ili kuwapatia haki ya msingi ya Cheti cha kuzaliwa watoto wao.Aidha aliongeza kuwa kampeni hii ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano itaanza machi 20 mwaka huu hadi april 07 mwaka huu na kuendelea kwa siku 90.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.