• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

PROGRAMU ya Imarisha Uchumi na Mama Samia yazinduliwa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 28th, 2024

Programu ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi inayoitwa Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) imezinduliwa mkoani Ruvuma kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

 Uzinduzi huo umehusisha mkutano wa viongozi wa Mkoa,wakuu wa Wilaya,Makatibu Tawala wa Wilaya,waratibu wa uwezeshaji ngazi ya Mkoa na Halmashauri na viongozi wa majukwaa ya uwekezaji wanawake kiuchumi wa Halmashauri zote.

 Programu hiyo pia imehusisha mkutano wa wajasiriamali wote Pamoja na viongozi,mkutano ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa  parokia ya Bombambili mjini Songea.

Akizungumza  kwenye nyakati tofauti kwenye Uzunduzi huo katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na ukumbi wa Parokia ya Bombambili, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng’i Issa amesema  IMASA ni programu ambayo inatekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

Amelitaja lengo kuwa la IMASA kuwa ni  kuimarisha uchumi wa wananchi na kwamba Baraza la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linasimamia  Programu hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo amewataja watekelezaji wakubwa wa programu hiyo ni Mkuu wa Mkoa ,Mkuu wa wilaya na Halmashauri zote.

Hata hivyo amesema IMASA imebuniwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Ikulu ambapo Baraza la Uwezeshaji linafanya kazi kwa kushirikiana na Mshauri wa Rais ambaye anashughulikia masuala ya wanawake,Vijana na Makundi Maalum.

“IMASA ni matakwa na maoni ya Mheshimiwa Rais,ambaye amedhamiria kuwasaidia wananchi kwa kupitia Ofisi za wakuu wa mikoa’’,alisema.

Hata hivyo amesema program hiyo itatekelezwa katika awamu mbili,ambapo katika awamu ya kwanza zinahitajika takwimu za wananchi waliopo mkoani Ruvuma na mikoa mingine ambapo unatumika mfumo wa kidigitali ambao utamwezesha mwananchi mwenyewe kuingiza taarifa zake zote muhimu.

Amesema wananchi wakati wanaingiza taarifa zao zitakuwa zinaonekana moja kwa moja kwenye mfumo hivyo kuonesha idadi kamili ya watu waliojisajiri ambapo amesema uzinduzi unaofanyika Ruvuma umefikisha mikoa nane hadi sasa iliyopitiwa na IMASA.

Amesema katika Mkoa wa Ruvuma usajiri utafanyika kwa wiki mbili  kwenye mfumo ambapo baada ya zoezi hili itatengezwa program maalum kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni wanawake,vijana na wenye mahitaji maalum.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres Magiri  ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kujisajiri kwenye mfumo.

Amesisitiza kuwa mfumo huo utawezesha upatikanaji wa kanzidata na taarifa mbalimbali za makundi na watu binafsi  wanaojihusisha na kazi mbalimbali za kiuchumi ili waweze kuwezeshwa kiuchumi kupitia IMASA.

Ameutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa wananchi wake wanajishughulisha na kazi mbalimbali za kuchumi zikiwemo kilimo,uchimbaji madini,uvuvi,ufugaji  na usindikaji wa bidhaa mbalimbali.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Viwanda,Uwekezaji na Biashara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Martin Kabaro amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022   serikali ilitoa mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 2.56 kwa  vikundi 327 vya wanawake,vijana na wenye ulemavu.

Amesema serikali pia ilitoa mikopo ya Zaidi ya shilingi bilioni 1.3 kwa vikundi 164 vya wanawake,vijana na wenye ulemavu hadi kufikia  Machi 2023.

Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma Januari 2024 umepokea mashine 20 za kukamua alizeti  zilizonunuliwa kwa ajili ya  vikundi 20 vilivyopo katika Halmashauri za Ruvuma.

Wajasirimali wadogo wakiwa kwenye  mafunzo ya Programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia kwenye ukumbi wa  Parokia ya Bombambili mjini Songea


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.