• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS Samia atoa magari 13 mapya kwa sekta ya Afya Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: February 16th, 2024

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya magari  13 kwa ajili ya kubebea wagonjwa na kufanyia usimamizi shirikishi katika sekta ya  Mkoa wa Ruvuma.

Hayo yamesema na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis Chomboko kwenye hafla ya kukabidhi magari sita mapya,iliyofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Chandamali mjini Songea ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.

“Awamu ya kwanza tulipokea magari saba na leo katika awamu ya pili tumepokea magari sita ili kutimiza lengo la magari 13 kati ya hayo magari tisa ya kubebea wagonjwa na magari  manne ya usimamizi’’,alisema Dkt Chomboko.

Akizungumza baada ya kukabidhi magari hayo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  ametoa rai kwa watumishi wakiwemo madereva kuyatunza magari hayo kwa kuwa serikali imetumia fedha nyingi kuyanunua.

“Haitakuwa na maana yeyote baada ya miezi michache magari yanaharibika,hata nia njema ya Mheshimiwa Rais ya kuwasaidia watanzania itakuwa haina maana,naagiza magari yatumike kwa malengo yaliyokusudiwa,yasiwe magari ya kubebea mbolea Kwenda shambani au kubebea nyasa’’,alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho akizungumza kwenye hafla hiyo amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri katika sekta ya afya mkoani Ruvuma.

Amesema hivi sasa Halmashauri zote nane zina magari mapya ya kubebea wagonjwa hivyo kupunguza changamoto ya magari kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amezindua kampeni ya chanjo ya surua na Rubella ambayo imeanza Februari 15 na inatarajia kukamilika Februari 18,2024 ambapo  zaidi ya Watoto 200,000 wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miezi 59 wanatarajia kupata chanjo hiyo.

Ugonjwa wa surua Rubella upo mkoani Ruvuma ambapo takwimu za mwaka 2023 zinaonesha kuwa sampuli 135 zilipelekwa maabara,ilibainika kuwa sampuli 22 zilithibika kuwa na virusi vya ugonjwa wa surua Rubella.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.