KATIBU Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Stephen Mashauri Ndaki amefanya ziara ya kikazi ya siku moja wilayani Nyasa ambako amekagua maendeleo ya miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Nyasa.Ndaki baada ya kufanya ukaguzi huo ameridhishwa na maendeleo ya Utekelezaji wa mradi huu na amemtaka Fundi anayejenga SUMA JKT kuharakisha ujenzi kwa kujenga usiku na mchana ili uweze kukamilika na kutumiwa na Mkurugenzi kwa kuwa uhitaji ni Mkubwa sana.
Katibu Tawala akiwa Wilayani hapa ametembelea Mradi wa ujenzi wa Wodi tatu za Watoto, wanawake na wanaume zinazojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa, Ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, Ujenzi wa Fensi ya Nyumbana Ofisi ya mkuu wa Wilaya, na amefanya kikao na Wakuu wa Idara na Vitengo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.
Aidha ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo na kuwataka Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia miradi ambayo Serikali imetoa Fedha na kumaliza haraka iwezekanavyo na kuzingatia ubora wa miradi hii.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.