Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameuagiza uongozi Wilaya ya Nyasa na RUWASA kuhakikisha Bibi Maria Ngairo Mkazi wa Mwerampya Kata ya Lituhi Wilaya ya Nyasa ambaye ametoa bure eneo la kujenga shule ya msingi na eneo la kujenga mradi mkubwa wa maji apewe maji ya bomba bure na kutunukiwa cheti.
Kanali Thomas ametoa agizo hilo wakati anazungumza mara baada ya kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Mwerampya Lituhi ambao Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 6.5 kutekeleza mradi huo unaotarajia kukamilika Aprili 2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.