klabu ya RAS Ruvuma imekabidhi jumla ya makombe manne kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed iliyoyapata katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo(SHIMIWI) Taifa yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa makombe hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza klabu hiyo kwa kuwa na mipango na mikakati iliyowezesha kupata ushindi wa makombe na medali hizo.
Naye katibu wa Klabu ya RAS Ruvuma Sports Ndg.Onesmo Mpuya amebainisha kuwa klabu hiyo imeweza kushinda jumla ya makombe manne na medali nne katika Mashindano hayo.
"Katika michezo yote tuliyo shiriki tuliweza kupata ushindi wa makombe manne na medali nne, moja ya dhahabu na 3 za Silva" Alisema.
Katika mashindano ya SHIMIWI 2024 Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma iliweza kushiriki michezo 6 ambayo ni riadha, kurusha tufe, dart, bao, baiskeli na karata.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.