MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amehudhuria Sikukuu ya Kumbukizi ya kuzaliwa Mtume Mhamad S.A.W katika Msikiti wa Wilaya ya Songea.
Akizungumza katika Sikukuu hiyo amesema kumbukizi hiyo inafanyika kila mwaka mara baada ya kuzaliwa Mtume Mohamed kwa Waislam.
Thomas amewashukuru viongo wa Msikiti huo kwa mwaliko na kuwa na ushirikiano na Serikali ikiwa kila mwaka wananpoadhimisha Sikukuu ya Kumbukizi ya kuzaliwa Mtume wanatoa mwaliko katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya na uhai niwashukuru pia viongozi wa Msikiti kwa mwaliko ikiwa hata mwaka jana mlileta barua ya mwaliko katika ofisi yangu”.
Katika Sikukuu hiyo amehamasisha harambee ya ujenzi wa Msikiti wa Wilaya unaotarajiwa kujengwa kwa shilingi milioni 300.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.