Mkoa wa Ruvuma umeendelea kupiga hatua katika sekta ya viwanda na biashara ambapo Mkoa una viwanda vikubwa sita vinavyoshughulika na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Viwanda vitatu vya kukoboa kahawa vipo Wilaya ya Mbinga, kiwanda cha kubangua korosho kipo Wilaya ya Tunduru, kiwanda cha kufua umeme kipo Wilaya ya Songea, na kiwanda cha kusindika unga wa sembe kipo Wilaya ya Songea.
Mbali na viwanda hivyo vikubwa, Mkoa wa Ruvuma una viwanda vya kati 25 vinavyoshughulika na usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo kama unga wa sembe, mchele, mikate, na maziwa.
Pia, Mkoa una viwanda vidogo 190 na viwanda vidogo sana 3,264 vinavyoshughulika na shughuli mbalimbali kama kukoboa na kusaga nafaka, kukamua mafuta ya alizeti, usindikaji wa mihogo, cherehani, usindikaji wa nyama, sembe, juice, useremala, na bidhaa nyingine za mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, na maliasili.
Bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo huuzwa ndani ya Mkoa na mikoa jirani kama Mbeya, Lindi, Mtwara, Njombe, Dar es Salaam, na nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Katika sekta ya biashara, Mkoa umeendelea na zoezi la kurasimisha biashara na kutoa leseni kwa kuzingatia sheria na kanuni za utoaji wa leseni za biashara kama ilivyoagizwa na Serikali.
Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2024, jumla ya leseni 8,370 zilitolewa na jumla ya milioni 783,926,622 zilikusanywa kama mapato ya ndani yatokanayo na utoaji wa leseni za biashara katika Mkoa wa Ruvuma.
Hatua hizi zinaonesha jinsi Mkoa wa Ruvuma unavyoendelea kuimarisha katika sekta ya viwanda na biashara
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.