Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wote nchini ambapo Serikali za pande zote mbili zimekubaliana hali ya biashara kote nchini kuendelea kama kawaida ili kuwapa watanzania huduma wanazostahili. Kwa maslahi mapana ya nchi.
Akisoma maazimio ya serikali na uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara Thobias Makoba
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali
Dodoma, amesema kwamba, kwa takribani siku 4 sasa kumekuwa na majadiliano kwa ngazi mbalimbali kati ya Serikali na viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara hapa nchini.
Amesema Mazungumzo haya yalitokana na madai na hoja takribani 41 ambazo wafanyabiashara waliziwasilisha serikalini ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Kutokana na hoja hizo, na baada ya vikao na mawaziri wa sekta husika, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia falsafa ya R 4 za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa ile ya Reconciliation kwa maana ya maridhiano, Leo tarehe 27 June, 2024 amehitimisha mazungumzo hayo hapo Dodoma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.