• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yaanzisha rasmi Hifadhi ya Mbambabay

Imewekwa kuanzia tarehe: November 13th, 2022

Serikali mkoani Ruvuma  kwa kutambua umuhimu wa uhifadhi umewakabidhi  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) hati ya kukabidhiwa visiwa vya Lundo,Mbambabay na  milima ya Mbamba na tumbi,yenye jumla ya hekari 597 kwa ajili ya uhifadhi.

Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekabidhi hati ya kumilikishwa eneo hilo ambapo pia amezindua uwekezaji wanyamapori katika kisiwa cha Lundo ambapo tayari wamewekwa wanyamapori jamii ya swala na ndege.

Kanali Laban amesisitiza kuwa kupelekwa kwa wanyama katika kisiwa hicho,kutasaidia kuongeza vivutio kwa watalii kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana wilaya ya Nyasa  na  Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla

Mkuu wa Mkoa amewaagiza wadau wa utalii na uhifadhi wakiwemo TAWA  na TANAPA   kuchukua jukumu la kutoa elimu ya uhifadhi na utalii kwa wananchi hasa wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu umuhimu wa sekta ya utalii katika kuchochea uchumi sanjari na kufungua vituo vya utoaji taarifa za utalii katika kila Halmashauri.

Akizungumzia historia ya kivutio cha utalii ambacho ni kisiwa cha Lundo chenye ukubwa za hekta 20,Mganga Mkuu Mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Dk.John Paparika ambaye pia wazazi wake wametokea katika Kisiwa hicho anasema kisiwa kimepewa jina la Lundo kwa sababu watu wa kwanza waliovuka kisiwa hicho kwenda ng’ambo ya pili walifikia kijiji cha Lundo.

Anasema kisiwa hicho tangu zamani kilikuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa vijiji vya Lundo,Ngindo na Chinula kwa sababu wakati wa vita ya Majimaji vilivyotokea kati ya mwaka 1905 hadi 1907 watu walikuwa wanakimbilia katika kisiwa hicho ambacho kina maeneo ya maficho.

“Baada ya vita ya Majimaji kuanzia mwaka 1908 kisiwa hiki kilitumika na wakoloni wa kijerumani kuwahifadhi watu waliopata ulemavu kutokana na ugonjwa wa ukoma ambao baadaye walihamishiwa katika kisiwa cha Puulu’’,anasema Dk.Paparika.

Hata hivyo anasema watu hao wenye ukoma walipandiwa matunda ya aina mbalimbali katika kisiwa hicho yakiwemo maembe, mapera,mananasi,machungwa na migomba ambapo hadi sasa katika kisiwa hicho kuna masalia ya miembe mingi na makaburi.

Anasema licha ya watu hao wenye ukoma kutengwa katika kisiwa hicho ,bado ndugu zao kila wiki walikuwa wanafika katika kisiwa hicho kuwatembelea na kuwaletea vyakula kwa kuwa kutokana na ulemavu waliopata walikuwa hawawezi kufanyakazi hivyo walihitaji msaada.

Historia ya kisiwa hicho,inaonesha kuwa kisiwa  kilisaidia wakati wa mgogoro wa kutoelewana baina ya kabila la wamatengo wa Wilaya ya Mbinga na Wanyasa wa Mwambao mwa ziwa Nyasa ambapo wamatengo walipokuwa wanashuka na silaha zao wakazi wa kata za Lundo na Mbambabay walikuwa wanakimbilia kujificha katika kisiwa hicho.

“Kwa kuwa wamatengo hawana uwezo wa kuogelea wala kuendesha mitumbwi,hivyo walikuwa wanashindwa kuwapata wanyasa ambao walikuwa wanapiga kasia na kujificha katika kisiwa cha Lundo’’,anasema Dk.Paparika.

Anasema kisiwa hicho kina utajiri wa aina mbalimbali za samaki wa mapambo ambao wanapenda kuishi sehemu za mawe.Inakadiriwa samaki mmoja wa mapambo katika nchi za Ufaransa,Ujerumani na Afrika ya Kusini anauzwa kati ya dola za Marekani 400 hadi 500 sawa na zaidi ya sh.milioni moja kwa samaki mmoja.

Mshauri wa Maliasili na Utalii Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema hifadhi ya Mbambabay  ina ukubwa wa eneo la hekta 597 na kwamba maeneo hayo yanafaa kwa kufuga wanyamapori na ndege.

Hata hivyo anasema Kati ya hekta hizo, mlima Mbamba una eneo lenye ukubwa wa hekta40,mlima Tumbi hekta 110,kisiwa Mbambabay kina hekta 27, kisiwa cha Lundo  kina ukubwa wa hekta 20.

“Milima na visiwa hivi vimejaaliwa kuwa na uoto mzuri wa miombo,mawe yanayozunguka visiwa hivi na milima kando kando ya ziwa yana hifadhi samaki adimu wa mapambo zaidi ya aina 400’’,anasisitiza Challe.

Kwa mujibu wa Challe,eneo la hifadhi ya Mbambabay ni muhimu sana kwa upande wa Tanzania  hususan katika matumizi ya shughuli za utalii kama vile utalii wa kuvua samaki,kupiga mbizi,yatching,utalii wa kuendesha mitumbwi na kuweka kambi kwenye fukwe.

Mtalaam huyo wa uhifadhi anasema eneo hilo likihifadhiwa litatumika kwa ajili ya mazalia ya samaki na hivyo kuongeza kipato kwa wananchi wanaotegemea shughuli za uvuvi.

“Mbambabay ikihifadhiwa inaweza kuleta ushindani kibiashara kwa sababu katika nchi yetu hakuna eneo linaloweza kutoa mchanganyiko mzuri wa huduma za kitalii kama zitakazotolewa katika eneo hili’’,anasisitiza Challe.

Wilaya ya Nyasa inaongoza katika Mkoa wa Ruvuma kwa kuwa na vivutio vya aina mbalimbali vya utalii.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  Mkoa wa Ruvuma

Novemba 13,2022

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.