Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amesema Halmashauri tatu katika Wilaya ya Songea zimekamilisha kwa mafanikio makubwa kazi ya kujenga madarasa 96 ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Mgema amesema hayo baada ya kukagua madarasa 29 kati ya 76 yaliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
“Sisi Wilaya ya Songea tumekwishafanya kazi tuliotumwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tumeikamilisha kwa mafanikio makubwa “,alisema
na kuongeza kuwa wanafunzi wote watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 watapata mahali pazuri pa kusomea.
Amesema madarasa yote 96 yaliyojengwa Wilaya ya Songea kwa gharama ya shilingi bilioni 1.9 .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.