• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAKUKURU Ruvuma yabaini mapungufu miradi mitano ya maendeleo

Imewekwa kuanzia tarehe: August 21st, 2023

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Ruvuma imebaini mapungufu kwenye miradi mitano ya maendeleo  yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3.7.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa wanahabari katika kipindi cha kuanzia Machi hadi Juni,2023,kwenye ukumbi wa TAKUKURU Mahenge mjini Songea,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda  amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuondoa mapungufu kwenye uchunguzi huo.

“Tumefuatilia utekelezaji wa miradi kumi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.9,katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo miradi mitano yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3.7 ilikutwa na mapungufu nah atua zilichukuliwa kuondoa mapungufu hayo’’,alisema.

Mkuu wa TAKUKURU ameitaja miradi yenye mapungufu kuwa ni mradi wa maji katika vijiji vya Masuguru na Mchoteka wilayani Tunduru unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.4 ambapo ameitaja changamoto iliyobainika kuwa ni ucheleweshaji upatikanaji vifaa  ambapo RUWASA imeshauriwa kutafuta malighafi mapema.

Miradi mingine ameitaja kuwa ni ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya sekondari Limbo wilayani Nyasa unaogharimu shilingi milioni 150 na kwamba mradi upo nyuma ya wakati ambapo Kamati ya Usimamizi wa mradi ilishauriwa kufanya kazi kwa haraka ili kukamilisha mradi huo.

Mkuu wa TAKUKURU ameitaja miradi mingine iliyochelewa kukamilika kuwa ni mradi wa matengenezo ya muda ya barabara za Liula-Mhongozi yenye urefu wa kilometa 13.99, barabara ya Matiri,Kindimba juu hadi Mkongotingisa yenye urefu wa kilometa 26.3,barabara ya Ngeruka hadi Matiri yenye urefu wa kilometa 25.16,ujenzi wa daraja la Mto Kaudongo na ukarabati wa daraja la Mto Mnywamaji ambapo miradi yote imegharimu zaidi ya shilingi milioni 374.

Ameitaja miradi mingine yenye mapungufu inayosimamiwa na TARURA kuwa ni matengenezo ya barabara za Manispaa ya Songea ambazo zimetengewa zaidi ya shilingi milioni 250 na matengenezo ya barabara za wilaya ya Namtumbo ambazo zilitengewa zaidi ya shilingi milioni 567.

Hata hivyo Hamza amebainisha kuwa katika kipindi hicho TAKUKURU kupitia uelimishaji wa umma imeweza kuimarisha klabu za wapinga rushwa 61 za shule za msingi na sekondari,kuendesha mikutano ya hadhara 21,vipindi nane za redio,maonesho kumi na kuandaa Makala za uelimishaji tisa.

Amesisitiza kuwa kupitia uelimishaji umma idadi ya wananchi wanaokwenda TAKUKURU  kupata ufafanuzi wa changamoto mbalimbali imeongezeka.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • BODI ya kwanza ya maji yazinduliwa Tunduru

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.