• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA MADABA walivyojenga daraja la mawe kwa teknolojia rahisi

Imewekwa kuanzia tarehe: March 21st, 2023

WAKALA wa barabara za vijijini na mijini(TARURA) imekamilisha ujenzi wa daraja lililojengwa kwa teknolojia ya mawe katika mto Mgombezi  linalounganisha kijiji cha Lipupuma,Mgombezi na Chechengu katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Songea Bakari John alisema,daraja la mto Mgombezi lina urefu wa meta 25 na ujenzi kwa kutumia teknolojia ya mawe ni wa gharama nafuu na la kwanza kujengwa wilayani Songea.

Alitaja gharama za ujenzi wa daraja hilo ni shilingi milioni 152 tu na kueleza kuwa, kama wangejenga kwa kutumia zege  na chuma kama ilivyo kwa madaraja mengine basi serikali ingetumia zaidi ya shilingi milioni 500.

Alisema,kabla ya ujenzi wa daraja hilo wananchi walilazimika kupita kwenye daraja la miti lililojengwa na wananchi wenyewe,hata hivyo wakati wa masika halikuwasaidia kutokana na mto Mgombezi kujaa maji mengi na kukatisha mawasiliano kati ya upande mmoja na mwingine.

Alieleza kuwa, kujengwa kwa  daraja hilo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo kwani limetatua kero ya muda mrefu ya usafiri na usafirishaji wa mazao hasa mbao na Tangawizi.

Meneja huyo wa TARURA aliongeza kuwa, kazi iliyobaki ni kuendelea kufungua barabara za kuunganisha mashamba  ili kuwawezesha wananchi  kuendelea na shughuli zao za kilimo kwa urahisi.

Baadhi ya wananchi waliokutwa wakivuka katika daraja hilo,wameishukuru serikali  kwa uamuzi wake wa kujenga daraja la kudumu kwani kwa muda mrefu walikuwa wakiteseka kupita kwenye maji pindi wanapohitaji kuvuka upande mmoja kwenda mwingine.

Nuru Francis  mkazi wa Lipupuma alisema,walikuwa na hali mbaya  kwani walilazimika kupita kwenye mto huo wenye maji mengi  kila siku na wakati wa masika walishindwa kwenda kwenye shughuli zao za uzalishaji mali kutokana na mto huo kujaa maji.

Michael Brumo,ameipongeza serikali ya awamu ya sita  kuona umuhimu wa kujenga daraja katika eneo hilo kwa sababu ilikuwa changamoto kubwa kila wanapotakakusafirisha mazao yao kutoka shambani kwenda sokoni.

Robert Mbilinyi,ameishauri serikali kuendelea kujenga madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ambayo ni ya gharama nafuu na kuachana na ujenzi wa madaraja ya chuma ambayo wakati mwingine baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wanahujumu kwa kuiba vyuma na hivyo kuisababishia serikai hasara kubwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.