Na Gustaph Swai-RS Ruvuma
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Ruvuma umesaini mikataba ya matengenezo ya barabara kwa mwaka 2024/25 na Kampuni ya Kimango Engineering Company Limited.
Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, ikishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa, Kanali Ahmed Abbas Ahmed.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Silvester Chinengo, amesema Serikali imeidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 22.19 kwa ajili ya kutekeleza jumla ya kilometa 1,170 za barabara Mkoani Ruvuma.
Hata hivyo amebainisha kuwa tayari mikataba 50 yenye thamani ya shilingi bilioni 14 imesainiwa, na utekelezaji wa miradi hio utaanza muda wowote kuanzia Sasa .
"Hadi sasa tumeingia mikataba 50 ambayo ina thamani ya bilioni 14 ,na utekelezaji utaanza muda wowote kuanzia Sasa, zoezi linalofuata baada ya hatua hii ni kuwakabidhi wakandarasi kazi kwenye maeneo ya wilaya zetu ambako ndiko kazi zinafanyika" amesema Mhandisi Chinengo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kimango Engineering Company, Happyness Kimaro, ameahidi kufanya kazi kwa weledi na kwa kiwango cha juu, huku akiishukuru Serikali kwa kuongeza kiwango cha mikataba kutoka shilingi bilioni 10 hadi bilioni 50 kwa wakandarasi wazawa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas , amesisitiza umuhimu wa wakandarasi kufanya kazi kwa ubora unaolingana na thamani ya fedha.
Kanali Abbas amewataka wakandarasi hao kutoa taarifa endapo watakutana na changamoto ili ziweze kutatuliwa kwa haraka.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameisisitiza TARURA kutoa kipaumbele kwa wanaruvuma na kina mama wenye uthubutu katika miradi ya Mkoa , na kuhakikisha madeni ya wakandarasi yanalipwa ili kuwezesha wakandarasi kufanya kazi kwa weledi.
I katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024, TARURA Mkoa wa Ruvuma ilitia saini mikataba 41 ya matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja na makalavati yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 11.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.